Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikweteamewashangaa watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya,akiuliza kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri ikoje?
Aidha,Rais Kikwete amesema kuwa Katiba inayojali makundi yote ndani yajamii, kama ilivyo Katiba Inayopendekezwa, kamwe haiwezi kuwa Katibambaya.
Rais Kikwete ameyasema hayo nyakati tofauti leo, Ijumaa, Oktoba 10, 2014,wakati alipozungumza na wananchi katika maeneo mbali mbali ya Mkoa waMwanza, ambako anafanya ziara ya siku tatu ya kikazi kukagua nakuzindua miradi ya maendeleo.
Akizungumza na mamia kwa mamia ya wananchi mjini Kisesa ambako ameweka jiwe lamsingi la ujenzi kwa kiwango cha lami na Barabara ya Usagara-Kisesa,Rais Kikwete amewataka wananchi kuwapuuza watu wachache wanaodai kuwaKatiba Inayopendekezwa ni mbaya na badala yake wajiandae kuipigiakura ya kuikubali wakati ukiwadia.
“Sijui katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamiikama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa – wavuvi wamo,wajane wamo, wafanyabiashara ndogo ndogo wamo, akinamama lishe wamo,wakulima wamo, wafugaji wamo….kila mtu yumo. Akinamama ndio usisemekabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Hivi katiba mbaya inakuwa kama inayopendekezwa nakama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?
Rais Kikwete amewambia wananchi: “Watakuja watu kuwashawishi kuwa KatibaInayopendekezwa ni mbaya, wasikilizeni lakini tumieni akili yetu,kama ile hadithi ya mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuungamkono Katiba Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana.”
Kitajwa kwa makundi sio kupewa haki zao.....wanatajwa kisha wanaambiwa hakuna mahali pa kudai haki zao kama wasipozipata toka serikalini......!!!huu ni usanii aliozoea huu.......atutolee rasimu yake ya kisanii sanii hapa.asubiri kumaliza muda wake uliobaki atuachie nchi yetu.
ReplyDeleteKatiba nzuri ni ile waliotoa maoni yao wananchi na kupendekezwa na Mheshimiwa Warioba na siyo hiyo ya CCM mnataka kuwalazimisha watu kuikubali.
ReplyDeleteHIVI IKITOKEA WANANCHI TUKAIKATAA HII RASIMU YA KATIBA ZILE HELA WALIZO BUBUDA WATARUDISHAAAA/ AU NDO IMETOKA HIYO
ReplyDelete