Kama Siyo Milion 58 Simba Ingefungwa Bao Tatu na Yanga

MATAJIRI wa Simba wamefurahishwa na matokeo ya suluhu waliyopata dhidi ya Yanga na kusema bila kambi yao ya nchini Afrika Kusini wangeweza kufungwa si chini ya mabao 3-0 na Yanga.

Kabla ya matokeo hayo ya juzi Jumamosi pale Uwanja wa Taifa, Simba ilikuwa Afrika Kusini ambako iliweka kambi ya siku nane kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ulimalizika suluhu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ‘KD’, alisema kikosi chao  kilikuwa katika hali mbaya ya kuweza kupoteza vibaya mechi dhidi ya Yanga na wasingefanya jitihada hizo wangejikuta wanapata kipigo cha aibu.

Dewji ambaye ndiye aliyekuwa mmoja wa waratibu wa kambi hiyo, alisema Yanga kabla ya mchezo huo walikuwa katika morali nzuri kuliko Simba. Alisema kambi na gharama mbalimbali walizoziingia zimewagharimu zaidi ya Dola 350,000 ambazo ni sawa na Sh58 milioni.

“Hatukuwa katika hali nzuri, tulilazimika kutumia akili hiyo ya haraka kuinusuru klabu kupata kipigo cha aibu maana tuliangalia timu yetu kulinganisha na Yanga na kubaini endapo tusingeandaa ile kambi tungeweza kupata kipigo cha aibu cha si chini ya bao 3-0,”alisema Dewji.

Matokeo hayo yamewakera mabosi wa Yanga waliokuwa wanataka ushindi kuziba kelele za Simba huku wachezaji kilio chao ni kukosa Sh80 milioni walizoahidiwa endapo wangeshinda huku Simba nao wakikosa Sh100 milioni ambazo wangepewa kama wangeishinda Yanga.

“Tulipambana sana hasa sisi mabeki, lakini tatizo lilikuwa mbele katika umaliziaji tu, tulikuwa tunalala na fedha uongozi ulituletea Sh80 milioni taslimu na ukatuhoji nani akabidhiwe lakini ndiyo hivyo tumechemsha,” alisema kwa huzuni beki mmoja wa Yanga.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi ww uliangalia mechi au umeadithiwa, kwa mpira aLIOCHEZA YANGA JMOS NASHANGAA AKUFUNGWA NA SMBA, KOCHA WAO KAZI ANAYO

    ReplyDelete
    Replies
    1. NA KOCHA WA SIMBA PIA KAZI ANAYO,KWA MECHI 4 POINT 4 INA MAANA GANI?UGENINI KOTE WATACHEA KICHAPO.

      Delete
  2. mechi nne pointi nne aibu!!!! na okwi wao!!

    ReplyDelete
  3. Point 18 za ugenini wanakosa hivihivi,Yaani Simba ni lazima watakuwa wateja wa Stand united,Mbeya city,coastal union,Azam,Mtibwa.,HIZI MECHI NI LAZIMA WAFUNGWE.
    Okwi kawaletea gundu

    ReplyDelete
  4. Lakini Simba haina doa la 'KUCHAPWA' kama Yanga 'ILIVYOCHAPWA' na Mtibwa.... heri nusu shari kuliko shari kamili...........SIMBA WOYEEEEh!

    ReplyDelete
  5. kwani kuna mechi gani mmecheza ugenini mpaka mseme hamna doa?ngoja muanze mechi za ugenini ndo mtajua kama mna timu au uozo eti mnashangilia drooo hovyooooo!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. hooovyooooo sijapata ona timu kubwa inaenda nje ya nchi kuweka kambi na magharama makubwa kwasababu ya kuja toa droooo!!! halafu mashabiki yao walivyokuwa "MAMBUMBUMBU" kama rage alivyowaita yanashangilia!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. MMECHAPWA NA MTIBWA - ITIKIA 'NDIO MZEE'

      Delete
    2. Waache kushangilia wakati kutofungwa na yanga kwao ni ushindi?
      Hukumsikia Dewji alivyosema,wao kama sio Kutumia mil 58 kwenda .S.A.
      wangefungwa na Yanga, na amekiri kabisa hawakuwa vizuri.
      Anonymous 20/10 .4.31.nakuunga mkono.ila umesahau ndanda.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad