HATUA ya Bunge Maalumu la Katiba kuhitimisha kazi yake kwa kupitisha Katiba inayopendekezwa, imemjengea taswira mbili tofauti Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta.
Wakati wengine wakitafsiri matokeo ya kupata theluthi mbili kila upande ili kupitisha Katiba inayopendekezwa kuwa yamembebesha Sitta taswira ya mtu shupavu na shujaa, upande unaompinga unamuona msaliti na kiongozi anayeweza kusababisha kuibuka na kukua kwa ufa mkubwa miongoni mwa jamii...Je wewe Unamweka Katika Kundi lipi Kati ya Hayo Mawili ?
hatuna TIME ya kuongelea siasa
ReplyDeletehapa, we tuwekee mambo ya DIAMOND, WEMA SEPETU nk uone tunavyofunguka. Hayo ya akina SITA hayatuhusu lkabisa......
Mheshmiwa Sitta Samweli ni mtu shujaa sana na ni miongoni kati ya viongozi wachache sana hapa Tanzania. hakuna maneno ya kuongezea kwa sababu kila Mtanzania ameona kazi yake. Amenusuru Taifa na wafitini wanaojiita maprofesa kumbe ni waoga wanakimbia dhamana na majukumu waliyopewa na Watanzania. viva Sitta my next prezdaaa.
ReplyDeletemdau hapo juu unachekesha, ni ushujaa gani alioufanya, kweli ndugu uko gizani!!!!
ReplyDeleteAmani Tanzania ipo ila itaondolewa na watu km kina Samweli Sitta ambao hawana hata hofu ya mungu njaa zao zinawapelekea kufanya mambo ya kijinga. Sitta baba utaweka historia ya umwagaji damu Tanzania Hongeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa .
ReplyDeleteUDINI: Udini ni kile kitendo cha kubagua,kuwatenga,kuwanyanyasa na hata kuwatesa watu wa dini fulani tu huku watu wengine wakiendelea kuneemeka .Sio sahihi kusema nchini Uingereza kuna UDINI kisa tu nchi hiyo inafuata na kutii mambo kadhaa ya kanisa la Kianglikani,Siwezi kusema pia nchi ya Saudi Arabia ina UDINI kisa tu inafuata na kutii mambo kadhaa ya dini ya Kiislamu. Kwa kuwa katika kufanya maamuzi ya ummakatika taifa lolote huathiriwa na utamaduni wa Taifa husika si ajabu wala mwiko hata kidogo kwa taifa lolote kuingiliwa na mambo ya UKRISTO au UISLAMU iwapo lego nikuipatia jamii maisha bora .Tanzania ni mfano wa kuiga kwani SERIKALI HAINA DINI ILA WANANCHI WAO WANA DINI .Hatushangai sikukuu za IDD na X-mass zikiwa siku za mapumziko na zikisherehekewa na WAISLAMU na WAKRISTO .Tutasema tu Tanzania hakuna udini pale watu wa dini zingine hawabaguliwi bali wanaheshimu kama wanavyoheshimiwa.. MAHUSIANO CHANYA YALIYOKO TANZANIA: [a]Viongozi wa dini kuhamasisha serikali iharakishe maisha bora kwa umma [b] Viongozi kuhamasisha wananchi wachague viongozi bora wala si bora viongozi [c]Viongozi wa siasa kushiriki shughuli za kidini bila kujali hizo ni dini zao au la [d] Viongozi wa dini kushiriki katika kumwapisha Rais mteule[e] Viongozi wa serikali/kisiasa kutumia BIBILIA/QUARAN wakati wa kiapo[f]Dua inayosomwa na Spika wa BUNGE kabla na mwisho wa vikao vya BUNGE. [g]Wimbo wetu wa taifa unatuombea Baraka [h]Katiba inatambua uwepo wa dini na MUNGU[MUNGU NI UWEZO UNAOWEZA NA USIOWEZWA NA KITU CHCHOTE] Ni vema tuepuke sana MAHUSIANO HASI:[a]Viongozi wa kisiasa kutumia siasa kupendekeza dini zao [b]Viongozi wa kisiasa kuwanyanyasa,kuwabagua na kuwatenga watu wa dini zisizo zao [c]Viongozi wa kisiasa kuwahadaa na kuwatumia watu wa dini fulani kwa lengo la kutaka kukubalika kisiasa au kushinda uchaguzi [d]Viongozi wa kidini kutaka waumini wao wachague kiongozi anayetokana na dini yao [e] Vyama vya siasa kuelemea kwenye UDINI ili hali sheria za kusajiri vyama vya siasa hairuhusu kuanzishwa CHAMA cha siasa chenye misingi ya DINI.Niombe tu hata kama hupendi soma tu RASIMU ILIYOPENDEKEZWA TOA HIZO DOSARI TUZIONE PIA VYOMBO VYA ULINZI VIIMARISHE ULINZI SIKU YA UZINDUZI KWANI MABEBERU NA WAKOLONI MAMBOLEO HATA LEO WAPO WANATUMIWA BILA KUJIJUA AU WANAJIJUA WAKIAHIDIWA MAKAZI BORA UGHAIBUNI.Kwa kuwa MUNGU yuko na Watanzania sala za HAYATI MWL J.K.NYERERE na SHEIKH ABEDI AMANI KARUME na RASHID MFAUME KAWAWA zitasikika na WATANZANIA WATAIBUKA KIDEDEA
ReplyDeleteWa tz bwana, wamelilia mabadiliko ya katiba wee, wamepewa nafasi hawataki kuitumia, unapokataa jambo tetea hoja sio kukimbia kwani unapokimbia ni dalili za kushindwa. sasa hawa ukawa hata kama wangekuwa na hoja za msingi nje ya bunge la katiba wasingeshinda walitakiwa wabaki bungeni kutetea hoja zao.
ReplyDeleteIbara mbili tu wametoka, sasa wanataka wafuatwe wanavyotaka wao tu kwa kuwa wao ndo wenye akili sana wengine mataahira au?? maana imekuwa kama mchezo sasa - kitu kidogo wamesusa - huo sio ukomavu wa kisiasa kabisa
na unaposema sita ataweka historia ya umwagaji damu naona si sahihi, kwani ukimwaga damu itasaidia nini? huo muda wa kumwaga damu si uutumie kufanya kazi zako za kuendeleza maisha yako na familia yako maana hakuna kiongozi yeyote atakaekuja kumtafutia kila mwananchi chakula ama mahitaji yake yote. hata baba yetu adamu alipoletwa duniani aliambiwa UTAKULA KWA JASHO LAKO kwa nini sisi tunataka tufanyiwe?!!!!!