Kibadeni: Phiri, Matola watimuliwe Simba, Uwezo Wao Umefikia Mwisho

 KOCHA wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni, amesema kuwa uongozi wa klabu ya Simba umekosea kuwasimamisha wachezaji Shaaban Kisiga, Amri Kiemba na Haroun Chanongo kwani tatizo lipo kwenye benchi la ufundi.

“Tatizo la Simba ni benchi la ufundi, tatizo si Chanongo wala Kiemba au hata Kisiga kama wanavyoona viongozi. Uongozi wa klabu ni mzuri, lakini wanatakiwa kujua kuwa hakuna jipya kwenye benchi la ufundi na ndiyo maana timu inafanya vibaya,” alisema Kibadeni.

“Kuwasimamisha wachezaji hao ndiyo kuiweka timu pabaya zaidi, inakuaje Simba ina wachezaji wazuri wa timu za taifa lakini wanapokuwa kwenye klabu wanashindwa kucheza vizuri?

“Nafikiri ni muda sasa timu ipewe makocha wazawa ukizingatia kuwa kuna wengi wamehitimu na wengine wameonyesha kufanya kazi inavyotakiwa kama Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Minziro wa JKT Ruvu.

“Uwezo wa Phiri na Matola umefika mwisho kwenye kuiokoa Simba, ubunifu wa ziada unahitajika ambao kwasasa hawana.

“Tatizo la viongozi wanaweza kuwa wanamtetea Phiri na mshauri wake ambaye ni Matola badala ya kuwatimua.”

Kibadeni ambaye pia ni mwanachama wa Simba,, aliongeza: “Mambo mengi yamebadilika, wakati Phiri akipata mafanikio na Simba pale awali, alikuwa na viongozi wanaomsaidia kwenye mambo ya nje ya uwanja huku ya ndani ya uwanja akiyafanya mwenyewe.”

Kibadeni ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake binafsi katika eneo la Chanika, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. POLENI SANA WAZEE WA MADOROO NA JKT RUVU LAZIMA WAWAFUNGE!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad