Maafisa wa utwaala nchini Liberia, wanasema kuwa watamshitaki mwanamume aliyepatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani wakimtuhumu kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu kukutana na jamaa wake aliyekuwa anaugua ugonjwa huo.
Mgonjwa huyo Thomas Eric Duncan alitakiwa kujibu maswali kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Marekani mwezi jana lakini maafisa wanasema aliulizwa ikiwa alikutana na jamaa yake mwenye virusi hiyo akasema la. Alisema hakuna jamaa yajke yeyote anaugua ugonjw ahuo.
Lakini waziri wa afya amesema kuwa mwanamume huyo alionekana akimpeleka jamaa wake mgonjwa hospitalini.
Bwana Duncan yuko katika hali mahututi, katika hospitali ya Dallas.
Ni mgonjwa wa kwanza wa Ebola kugudnulika nchini Marekani ambako zaidi ya watu 100 wanachunguzwa ikiwa wameambukizwa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3,330 wamefariki kutokana na Ebola katika nchi nne za kanda ya Afrika Magharibi.
Taarifa ya kutaka kumfungulia mashitaka mghonjwa huyo ilitolewa katika mkutano wa kila wiki wa serikali kuarifu waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini humo.
Liberia Kumshitaki Mgonjwa wa Ebola Aliyepatikana na Ugonjwa Huo Marekani
0
October 03, 2014
Tags