Lissu: Marehemu Amepiga Kura Katiba ya Sitta
2
October 16, 2014
MWANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema mchakato wa kutengeneza katiba mpya ni wa kihistoria kwani jina la marehemu lilipiga kura.
Akifafanua kauli hiyo alisema jina la mjumbe Shida Salum aliyefariki dunia Julai mwaka huu, limo kwenye orodha ya waliopiga kura ya ndiyo wakati kupitisha Katiba inayopendekezwa.
Lissu alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa alipotoa mada kwenye mdahalo wa kujadili Katiba iliyopendekezwa inayosubiri kupigiwa kura na wananchi, ambako alihoji ni Katiba Mpya au katiba ya kiimla katika rangi ing’aayo.
“Aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kundi la 201 kila mmoja anajua kwamba alifariki dunia lakini ukiangalia kwenye orodha ya waliopiga kura (huku akiionyesha kitabu kwa washiriki), anaonekana amepiga kura ya ndiyo.
“…Hii inawezekanaje jamani, ndiyo maana nakubaliana na Rais (Jakaya Kikwete) kuwa hii katiba iliyopendekezwa ni ya kihistoria,” alisema Lissu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kitendo cha baadhi ya wajumbe kupiga kura wakiwa hospitalini ni miongoni mwa matukio yatakayokumbukwa kwa kuweka historia kwani halijawahi kutokea sehemu yoyote ulimwenguni.
Tags
CCM are capable of doing anything jus to get what they want............fkthm
ReplyDeletehiiii ni hatari, wanafanya masihara mpaka kwa watu waliokufa? tena ningekuwa Zito Kabwe ingekuwa shidaaa, maanake huyo Shida salum ni mama yake mzazi.
ReplyDelete