Maswali 7 Ya Godbless Lema Kwa Polisi-Mauaji ya Mtuhumiwa wa Mabomu Arusha

1.Tobo la risasi katika hiyo picha Linaonekana tumboni. Je hapo ndipo lilipo ---- la kulia? kwanini wadanganje..?? what are they hiding?.

2.Nani mwenye uwezo wa kuthibitisha makosa ya mtuhumiwa na kukiri kwake kuhusika namatukio ya ugaidi?.

3. Hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma kwa maana ya mgongoni si tumboni.

4. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo"halafu umsafirishe bila kumfunga pingu?.

5.Kwa jinsi ambavyo nguvu kubwa ilitumika na Polisi wenyewe na hata Serikali nachama tawala kupotosha juu ya tukio lile la milipuko kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, na kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete aligomea wito wa Chadema na makundi mbalimbali ya kijamii wa kumtaka aunde tume ya kijaji (Judiciary commission) kuchunguza mauaji yale, kwa nini tuwaamini polisi kuhusu taarifa namaelezo yao kuwa mtuhumiwa alitoroka akiwa chini ya ulinzi kisha akauawa?.

6. Tukumbuke kuanzia mwanzo jeshi la Polisi na hata Rais hawakuonyesha nia njema katika hili leo hii tuwaamini walikuwa wana nia njema ya kumfikisha mtuhumiwa kwenye mikono ya sheria?.

7. Kifo cha mtuhumiwa katika"Mazingira tata" mikononi mwa watuhumiwa wengine (Maana hata polisi walituhumiwa kuhusika) lazima kitaacha maswali mengi bila majibuTunahitaji jeshi linalotoa huduma (PoliceService). nitakuwa wa mwisho kuamini tukio hili....... (Godbless Lema).
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kweli haijaniingia akilini kabisa, ikiwa watuhumiwa wa wizi kutoka gereza la segerea au keko wakiletwa mahakama ya kisutu au mahakama kuu wanafungwa pingu, iweje mtuhumiwa wa ugaidi asafirishwe kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine bila pingu!!!! Hili saga halina tofauti na lile la Miss Tanzania! Ni sheeederrr tupu TZ

    ReplyDelete
  2. mbuzi nyie hawakufa ndugu zenu lait kama wangekuwa ndugu zenu walikufa msinge hoji kwann yeye kafa apigwe tumbo, mgongo yote n mshahara wa dhambi

    ReplyDelete
  3. acha jazba anonymous 4:15, mshahara wa nini kwa mtuhumiwa?? hajathibitishwa!!! alomuua ni mtuhumiwa mwenzie (police)

    ReplyDelete
  4. Wewe lazima uwe na maswali mengi kwakuwa zamani ulikuwa mwizi wa magari pamoja na ujambazi ulikuwa unashirikiana na polisi ambao sio waaminifu ndio maana uajifanya unashangaa,huna lolote usituletee siasa hapa,waongee wengine sio wewe,kwa vitendo vyako uliuwa na kudhulumu wangapi alafu leo ujifanye wewe mwema?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad