Mwimbaji mashuhuri duniani ,Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.
''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown.
Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikimye.
Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.
Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema.
Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.
Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.
sasa kwani ni uongo hiyo ni kweli kwamba watu tunapunguzwa duniani kwani tumekua wengi sana hapana chezea illuminat planing
ReplyDeleteSio uongo wanataka kupunguza idadi ya watu sababu sio rahisi ku control watu wengi ila ni rahisi kuwa control wakibaki wachache hiyo ni trailor kidogo ya kitu inaitwa New World Order aka NWO so get ready
ReplyDelete