Matusi ya Mama Wema..Kajala na Wema Sepetu Watoana Jasho Polisi

Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

DURU ZA ‘KIUBUYU’
Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii.

MATRIDA MBARONI
Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema (Team Wema).
Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.

Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo.

KAJALA ACHOKA, AKIMBILIA POLISI
Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa.
RB
Gazeti hili lilifanikiwa kunasa namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomeka KJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA MATUSI MTANDAONI.

Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande mbili zikaanza.

KWANZA
Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba.

WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI 
Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo.

“Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani. Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa gharama yoyote.

“Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea,” alisema shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.

WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI   
Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria.

Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao.
Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo.

KAJALA NA KUNDI LAKE
Awali Kay alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa kituo.

Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa wake waliyeyuka.

WEMA AINGIA MITINI
Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana.

Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake.

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni Mama Wema alimtolea uvivu Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kay asiende jela na kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo kubwa.

Imeandaliwa na Hamida Hassan, Imelda Mtema, Mayasa Mariwata na  Shani Ramadhani.

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mama wema anajisahau sanaaaaa.

    ReplyDelete
  2. jaman kay jitahidi tu km vp urudishe hizo m13 zisikutoe roho bure. binadamu hawaelewi maana ya kutoa msaada...wanahisi ukitoa msaada basi ndo na ww usipate ili waendelee kukuekachini yao nyoooooooo. napitaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. ila na ww k hukuona mabwana mpaka ukalale na aliye mlala shoogaa akoooooo mxuuuuuuuuuuuuuu uchafu unawasumbua

    ReplyDelete
  4. KAJALA KM ANAPESA ATOE PESA ZETU ASILETE UKUUUMAA KABISA TENA ATAKOMAA ATOE HIYO PESA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hapo hata Wema aende mahakama gani kudai mil. 13 toka kwa Kay atashindwa,
      maana haikuwa mkopo,hata kama kutakuwa na mashahidi 100 walioona ni kazi bure.
      Halafu sidhani kama wema anadai hizo hela,wao wana mambo yao mengine.

      Delete
    2. KWIKWIKWIKWI ETI PESA ZETU. PESA GANI UNAYO WEWE KAMA SII USHABIKI TUU! LOHH, WENYE HELA UNAWAJUA WEWE! AU WASEMA TU PESA ZETU PESA ZETU. MIL 13 ZINAWATOA ROHO, HUYO WEMA ALIZITOA ILI KUJIONYESHA KWA WATU WALA SII KWA MAPENZI, HELA ZENYEWE ZA KUHONGWA

      Delete
  5. Issue sio pesa bana kwani mama wema anamdai kajala nawazazi wa kajala wametukanwa kwa lipi ni kukosa adabu huko hamna mzaz anapenda mwanae aharibikiwe so hakupaswa kuwatukana

    ReplyDelete
  6. mtu mwenyewe a.k.a k sasa umeanza kujitukana mwenyewe kwa kujiita k !toka lini k ikawa na shukrani hata akilipa mil 13 hawezi kulipa utu WEMA hauozi wala haulipwi!msenge ndio nshema huko mabatati atatupeleka wengi!

    ReplyDelete
  7. Hii habari ya mil.13 ni wapambe tuu wanakuza,kwani Wema hajatamka kama anadai,na nakumbuka kwenye mahojiano fulani Kay alidiriki kusema atamuheshimu Wema siku zote za maisha yake kwani kitendo alichofanya cha kumtoa jela
    anakithamini sana.

    ReplyDelete
  8. Kay hawezi kushindana na Wema kwa lolote,kwani tabia zao hazifanani.
    Si unyamaze tuu,mwenzio anaongea kama kawashwa kiberiti,we mwenzangu na mie maneno mawili tu kilio utafikiri umefiwa na mtu wa karibu,KAA KIMYA.
    Na kama ni Mil.13 basi waende mahakamani muamuliwe kisheria.Kaa kimya kajala,yaani natamani nije niongee na wewe siku moja lakini naogopa udaku.Narudia tena,KAA KIMYA KAY,uone wapambe watakutafuta kwa lipi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWELI MDAU,SIKU ZOTE MWEREVU NA MJINGA HAWAFUNGAMANI.ILA TATIZO LA KAJALA NAE HASIKII USHAURI.
      KWANI UKIKAA KIMYA KUNA NINI WEE WIFI YANGU KAJALA JAMANI ?

      Delete
  9. Ndiyo,dawa ya moto ni moto,
    Ukikaa kimya na wao watapiga kimya vinginevyo wataonekana machizi kuongea na bubu.

    ReplyDelete
  10. Hapo ni timu Wema na timu Kajala ambao ki ukweli wote ni wajinga,
    na ndio maana viongozi/watu wenye hekima wako kimya.Hawa watu wameanza kuchokoana siku nyingi kidogo lakini tunadhani hakuna watu wa busara wa kuongea nao?

    ReplyDelete
  11. 13 mil hakutoa wema.alitoa ck akijua tenda wema ujiwekee akiba.malipo ya yakawa penzi.tuambieni harusi ilikuwa lina hadi mdai kajala kachukua mume wa wema.huyo wema katembea na wanaume wangapi?leo hii awe msafi wa kuibiwa mume?

    ReplyDelete

  12. kajala jaribu kuachana na haya mambo ya mashindano tuone kipi kitafuata,japo
    umeumia sana kuvunja urafiki wenu,lakini ukweli wewe sio aina ya wema,achana nae bhana.
    wee huoni penny anavyofanya?Hawana shukrani kwani sikutegemea kama wangemng'ong'a Jokate kwenye B/day ya wema vile japo nadhani yeye Jokate hakugundua na kujipendekeza kwake,tangu lini watu mlionyang'anyana mwanaume mkapatana.pumba!

    ReplyDelete
  13. Haaaaaa nacheka mie jamani duu nawapa pole wote. Kajala vipi China?!! Sikusikii duuuu bwana kamwaga manyanga au kaishiwa hizi Pesa za kuhongwa. Kajala hayo mafao uliyobakiwa nayo yachezee utajuta!!! Alafu K we Mkubwa usishindane na mtoto Wa mama wema wote hakili hawana mtoto Wa njoka atazaa Samaki subili dai ampige chini mwaka juu utawaishia pabaya nyie 2

    ReplyDelete
  14. mbwaaa wewee ampige chini akutombe wewe amaa?????????????????sahau wema kuachana na diamond ndo kumekuchaa hivyooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad