Japokuwa jana niliangalia kwa muda mfupi Mchakato wa makabidhiano ya katiba ya CCM iliyooandaliwa na Sitta, Chenge,wabunge wengi wa CCM (ukiwaacha Lugola na Filikunjombe walioiasi) na mawakala wao, nilishtushwa kutowaona Mabalozi wa nchi wafadhili wa serikali ya CCM, wajumbe wote wa Tume ya Katiba na Maraisi Wastaafu Mh Benjamin Mkapa na Aman Abeid Karume. Je, tatizo ni mimi sikuwaona au ni kweli hawakuwepo? Na kama ni kweli hawakuwepo;
Je, ndo tuamini kuwa watu wote hawa muhimu wamesusia katiba ya CCM?
Je, huu siyo uthibithisho wa taarifa kuwa mabalozi hawa walimwambia JK haiafiki katiba hiyo?
Je, hii haimaanishi kuwa katiba ya fisadi Chenge na mbabaishaji Samwel Sitta inapingwa vikali hata ndani ya ccm yenyewe?
Ninatafakari tu kwa sauti wala sina ugomvi na mtu ye yote.
Nawasilisha,
By Aweda
Kina mkapa wana akili km wamekataa kweli kwani hata nyerere angekuwa hai hawa wasingefika hata robo.wizi mtupu kazi mabavu tu
ReplyDeletehata mke wa muasisi wa taifa hili, mama Maria Nyerere hakuwepo!! hapo pana shidaaaaa!!!
ReplyDeleteWamekataa cauz ni ubatili mtupu
ReplyDelete