Mtifuano Wa Katiba Mpya Wahamia Uraiani, CCM Kupata Kibarua Kigumu

Baada ya Bunge la Katiba juzi kufanikiwa kupata theluthi mbili ya wajumbe wa pande zote mbili za Muungano na kupitisha Katiba inayopendekezwa, sasa msuguano kuhusu Katiba unaonekana kuhamia uraiani.

Msuguano kuhusu Katiba hiyo unatarajiwa kuendelea mitaani, ndani ya vyama vya siasa na kwenye majukwaa kutokana na tofauti ya mitizamo iliyoibuka kuhusu Rasimu ya Katiba iliyopitishwa.

Ingawa matokeo ya kura za ushindi yalipokewa kwa furaha na wajumbe waliokuwapo bungeni kwa kucheza na kurusha vijembe kwa wapinzani, huenda kibarua kitakuwa kigumu kwa CCM itakapolazimika kupambana na wananchi, wanasiasa, wanaharakati na viongozi wa dini ‘waliojeruhiwa’ na mwenendo wa Bunge.

Bunge hilo liliendeshwa kwa upinzani mkali kutoka kwa makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wakitaka lisimamishwe kwa madai kuwa limechakachua maoni yao kama yalivyopendekezwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad