MWALIMU wa makomandoo katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 94 KJ kilichopo Ngerengere mkoani Morogoro, Luteni Octavian Mgowele (33), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke, Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkazi wa Buza jijini humo aliyetambulika kwa jina moja la Alkado maarufu kwa jina la Mbavu za Mbwa.
Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo ni kwamba komandoo huyo anatuhumiwa kufanya mauaji
hayo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, wiki iliyopita wakati akiwa Baa ya Mbondela iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo jana, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake alisema Luteni Mgowele anayedaiwa kuwa ni komandoo wa JWTZ alikuwa katika baa hiyo na mkewe ambaye jina lake halijafahamika pamoja na Alkado.
Shuhuda huyo alisema Mgowele ameoa hivi karibuni walikuwa wamekaa meza moja pamoja na Alkado wakiendelea kupata vinywaji. Alisema wakati wakiendelea kupata vinywaji ndipo Mgowele aliponyanyuka na kwenda chooni.
Ilielezwa kuwa baada ya kurejea alikuta mkewe amehama meza na baada ya kuhoji kwa nini amehama, ndipo mkewe akajibu kuwa Alkado alikuwa anamshika kiuoni ndiyo maana amehama eneo alilokuwa wamekaa mwanzoni.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo ni kwamba majibu hayo hayakumfurahisha Mgowele na akaamua kumvuta Alkado na kisha kuanza kumshambulia kwa kipigo ambapo alimtoa eneo alilokuwa amekaa na kumsogeza kwenye giza katika eneo hilo la baa.
Kutokana na kipigo anachodaiwa kupata Alkado kilisababisha baadhi ya watu waliokuwa kwenye baa hiyo kuingiwa wasiwasi kuwa huenda akamsababishia kifo. Hata hivyo, hakuna aliyeweza kwenda kusuluhisha maana mwanajeshi huyo alikuwa akiogopwa hasa kwa kuzingatia watu wengi wanajua ni komandoo na ni mwalimu wa makomandoo wa JWTZ.
Ilielezwa kuwa mwanamke aliyetambulika kwa jina la mama Rachel aliambulia kipigo baada ya kutoa taarifa kuwa kuna mtu anapigwa eneo hilo ambapo mbali ya kupigwa makofi inadaiwa alimwagiwa mchanga mdomoni kwa sababu ya kusema kuna mtu anapigwa na mwanajeshi huyo.
Taarifa zaidi zilidai baada ya kipigo hicho, Luteni Mgowele aliamua kuondoka na kuelekea
nyumbani kwake ndipo wananchi wa eneo hilo walipoamua kutoa taarifa polisi ambapo walifika na kumchukua Alkado ambaye wakati huo hakuwa na uwezo wa kuhema kutokana na kipigo alichokipata.
Ilielezwa kuwa Alkado alifariki dunia eneo hilo la baa baada ya kipigo ambapo kwa mujibu wa wananchi ni kwamba huenda alichanwa mbavu.
Hata hivyo, baada ya tukio hilo baadhi ya walinzi katika baa hiyo walisema Luteni Mgowele alirudi usiku ili kufahamu kinachoendelea lakini mwili wa Alkado ulikuwa umeondolewa katika baa hiyo ya Mbondele.
Mwili wa Alkado umehifadhiwa Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam na jana madaktari wa hospitali hiyo na madaktari wa Jeshi la Polisi walikuwa wakiufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo.
Akithibitisha kukamatwa kwa Luteni Mgowele, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Nyigiza Wankyoo alisema wanamshikilia Mgowele kwa tuhuma za mauaji na kwamba kesho (leo), hatua zaidi za kisheria zitachukua mkondo wake ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.
Alipoulizwa kwa nini asichukuliwe hatua za kijeshi, Kamanda Wankyoo alisema kutokana na
tuhuma ambazo zinatolewa dhidi ya Luteni Mgowele, tuhuma zake zitasikilizwa mahakamani
huku akifafanua jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa wakili wa Serikali.
Kuhusu madai kuwa baadhi ya wanajeshi wamemtorosha mwanajeshi huyo kituo cha polisi,
alisema hazina ukweli wowote na kwamba mwanajeshi huyo anashikiliwa na sheria itachukua mkondo wake.
Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ , Joseph Masanja alipoulizwa iwapo ana taarifa za kukamatwa kwa mwalimu huyo wa makomandoo wa jeshi hilo, alisema hawana taarifa hizo lakini aliahidi kufuatilia ili kubaini kama zina ukweli au la.
"Hatuna taarifa za tukio hilo, tutafuatilia na kisha tutatoa taarifa rasmi," alisisitiza wakati akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo, ni kwamba mwili wa marehemu Alkado unatarajiwa kusafirisha kesho kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko. Kwa sasa msiba upo eneo la Mwembe Yanga, Dar.
Mwalimu wa Makomando wa Jeshi la Tanzania Afanya Mauaji Baada ya Mkewe Kushikwa Kiuno
2
October 17, 2014
Tags
Poleni sana wafiwa.Sifurahii mtu kuwawa ila mara nyingi mambo haya huwa na maafa hasa pale mkosaji huwa hataki kukiri kosa na kuomba msamaha badala yake huwa anajibu jeuri.Hii humfanya mkosewaji kupatwa na uchungu na kupungukiwa na maamuzi ya busara na kupelekea majuto baadaye.Tuheshimu vya watu na tuchunge midomo yetu pia kuepusha matukio ya aina hii kujirudia rudia.
ReplyDeleteHayo Ndiyo mambo ya Mboo kubwa kuma kwa jirani :-)
ReplyDelete