Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Afukuzwa Kazi, Said Hassan Said Apewa Nafasi hiyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1)cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

My Take:
Hii ni Kama: Nakufukuza kazi kwa sababu umetumia demokrasia yako vibaya kwa kupiga kura ambayo siitaki!
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana Othuman bila shaka uliyajua haya tangu mapema lakini uliendelea kushikilia msimamo wako hukuogopa ngendebwe za mafisadi wa sisiemu na vibaraka wao walioko hapa zanzibar. wewe kwetu ni mshindi wa demokrasia na kwa hakika watu kama wewe ndio hasa watakaoikomboa zanzibar yetu kutoka katika mikono ya wakoloni weusi (ccm)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wee nawe kalale,unajua maana ya ukoloni?

      Delete
  2. UKItaka KAZZZZZIIIIII LAZIMA UWWWEEEEEE CCCCCCCMMMM..................!!!!! hiyo ndiyo duemokirasiaaaaa ya kibongobongo!!!!!

    ReplyDelete
  3. hi ni mbaya, ila ukishaamua kuwa mfuasi wa shetani usije ukaanza kuabudu mema, lazima shetani akufukuze kazi, kama uliokoka ukamkataa shetani na kazi zake zote ni haki yako kuondoka huko.. al the best Othman

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad