Nani Alimuelewa Mh.sitta Aliposema Wanataka Kujadiliana na Walio Piga Kura ya Hapana Bunge la Katiba

Wakati wa kipindi cha bunge Jana, kama ambayo wengi wenu humu mlimsikia, mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh. Samwel Sitta alisema ameunda kamati ya maridhiano kwa lengo la kukutana na kujadiliana na wajumbe waliopiga kura ya hapana kwa ibara zote za katiba siku ya jana na aliongezea kuwa sio kitu cha kawaida kwa mtu kukaa muda huo waote bungeni alafu apige kura ya hapana. Ambacho sijakielewa ni,lengo la kujadiliana na waliopiga kura ya hapana ni nini?Baadaya ya mjadala,ina maana wanaweza kupewa fursa ya kupiga kura tena kama watabadili misimamo yao?Ana maana kuwa pia UKAWA walikuwa sahihi kutohudhuria vikao kwani wangeshiriki alafu siku ya mwisho wakapiga kura ya hapana wangeonekana wa ajabu na wangeundiwa kamati ya maridhiano?nilijiuliza maswali mengi bila majibu,walau nianze na haya kwa mwenye ufahamu wa kile kinachoendelea ukizingatia kuwa kuna waliopiga kura ya hapana kwa siri,nao wanatakiwa wahudhurie kikao cha maridhiano au ni vipi?
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mboma ni kitu Rahisi the right of minority should be considered too...the true meaning of democracy....its very pocble Ahao.wahapan wakawa wako ryt basing on many factors...!

    ReplyDelete
  2. Watanzania nani ametuloga? Hapana kweli kibok haya ngoma tuangaalie party two nayo vipi

    ReplyDelete
  3. jamani jamani jamani tutafika kweli..!!

    ReplyDelete
  4. Mimi sijamuelewa na sitakaa nimielewe....huyu mzee Sitta naona tayari ameshapata matatizo ya akili sasa na anatakiwa matibabu ya haraka sana kabla hajaendelea kupata madhara zaidi.anachofanya ni wehu wa waziwazi mchana....mjumbe ameshasema hapana kwa ibara zote meaning kwamba rasimu yote ni uchafu kwake kwa sababu imechakachuliwa vipengele vyote vyenye kuibeba rasimu so haina maana kumuundia kamati mtu huyo...kinachoruhusiwa na kanuni za bunge la katiba ni kuunda kamati ya maridhiano kama kuna vipengele vichache kwenye baadhi ya ibara vimekoswa kuungwa mkono na sio rasimu yote na mwisho wa siku marekebisho yatfanyika kwenye vipengele hivyo tu ili kupata muafaka....sasa kama mtu kakataa rasimu yote kamati ni ya nini?!!kwamba anataka kuanza kupitia tena rasimu yote upya?!au ni kumtishia mjumbe maisha kama wanavyofanya sasa?!na hata wakifanikiwa kumtisha na kumbadili msimamo wake haina maana tena as ansard ya bunge tayari imesharekodi kura ya hapana kwa mjumbe husika.....kubadilisha maamuzi ya mjumbe inawezekana tu Tanzania na not anywhere else.....poor Sitta.....atakufa kwa kihoro kwa kushupalia mambo asiyoyajua na sasa Kikwete na wenzake waliomuwekea mtego wa kummaliza kisiasa qako pembeni wakimcheka kwa kejeli huku wakigonga cheers kwa mbaaaali na glass zao za mvinyo na whisky.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad