Nicki Minaj na Boyfriend wake Wamwagana? Boyfriend wake Afunika Tattoo ya Minaj

Wanasema dalili ya mvua ni mawingu, hivi ndivyo inavyoonekana katika uhusiano wa Nicki Minaj na mpenzi wake Safaree Sam ambaye alikuwa amejichora tattoo yenye picha ya Nicki na jina lake pia.

Wiki hii, Safaree ameonekana akiwa kifua wazi huku akiwa ameifunika tattoo ya picha ya Nicki na jina lake kwa michoro mingine. Tattoo nyingine aliyokuwa ameichora mkononi mwake inaonekana pia ikiwa imefifia sana ikiashiria kufutwa.

Hali hii imechochea kuni tetesi zilizoanza kusambaa kuwa wamepigana chini hasa baada ya Nicki Minaj kutweet, “Single and Ready to mingle.”

Tweet ambayo kwa mujibu wa Urban Islandz haikuwa na kwa ajili ya uhusiano wake bali alikuwa anazungumzia muziki wake kuwa anayo nafasi zaidi kwa mashabiki wake wakiume

Inaelezwa kuwa huenda Nicki hakutaka attention kama alivyofanya boyfriend wake huyo kujichora picha yake na ndio sababu ameamua kuifuta.

Itafahamika tu..endelea kutembelea tovuti hii tutakujuza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad