Baada ya vyama vinne vya upinzani nchini kusaini makubaliano ya kushirikiana pamoja na kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zote zijazo, umoja huo sasa unakabiliwa na kazi ngumu ya kuweka sawa mambo, ikiwa ni pamoja na mchakato wa kumpata mgombea urais, kabla ya filimbi ya uchaguzi kupulizwa.
Vyama hivyo vitalazimika kufanya uamuzi katika sera tofauti za vyama vyao, kukabiliana na Sheria ya Uchaguzi, taratibu za kupata wagombea wa kuanzia ngazi ya chini hadi urais na jinsi ya kuendesha kampeni zao kabla ya kuwaendea wananchi kuwaeleza kuwa wameshajizatiti kukabiliana na chama tawala, ambacho kina mtandao karibu nchi mzima uliojengwa kwa miaka mingi.
Vyama hivyo vimeibuka na nguvu mpya baada ya kuunganishwa na hoja ya kutetea Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilielezewa kuwa ilitokana na maoni ya wananchi na hivyo kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupambana na wajumbe wa CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Vyama hivyo, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD vilisusia mchakato wa Katiba kwa kile vilichodai kuwa ni kutoridhishwa na mambo yalivyokuwa yakiendeshwa na sasa umoja wao umekwenda mbali zaidi kutaka kushirikiana kwenye chaguzi.
Kutekeleza hilo, Jumapili iliyopita wenyeviti wa vyama hivyo, Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF), Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Dk Emmanuel Makaidi (NLD) walisaini makubaliano ya ushirikiano huo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Jangwani.
Moja ya kazi ngumu inayoukabili umoja huo ni jinsi ya kumpata mgombea wa urais atakayetoa upinzani mkubwa zaidi kwa mgombea wa chama tawala na kuendelea kupunguza kura za CCM baada ya mafanikio ya mwaka 2010 ya kupunguza asilimia 20 za kura alizopata RaisJakaya Kikwete mwaka 2005.
ebu nyie wapumbavu andikeni hivi vichwa vya habari vizuri, mnataka wananchi waanze waona UKAWA hawana maana, nani kasema wanagombania uraisi? hawa ni watu makini bwana, na wakati ukifika watamchagua mtu wao na kumsimamisha, nyie waandishi wa habari ndiyo mnayumbishaga mambo sababu ya matumbo yenu, pumbaf!!! ukisoma kichwa cha habari na habari yenyewe ni tofauti, Mungu atatubariki na watanzania watapata mabadiliko, VIVA UKAWA, VIVA TANZANIA!!
ReplyDelete