Raisi Jakaya Kikwete Afunguka ya Moyoni ..Asema Kazi ya Urasi ni Ngumu Anatamani Muda wake Uishe


Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru kufanya mambo yake, ikiwamo kilimo, huku akiamini atapatikana Rais bora kuiongoza vizuri zaidi Tanzania kuliko yeye.

Rais Kikwete alisema hayo Beijing alipokuwa akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha mataifa yao nchini China.

Kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Wageni wa Serikali ya China ya Diaoyutai, Rais Kikwete katika shughuli yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku sita kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Xi Jinping.

“Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu, nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha,” alisema Rais Kikwete kwenye mkutano huo baada ya naibu balozi wa Nigeria, Sola Onadipe kuelezea kushangazwa na kauli yake ya kutamani muda wake wa uongozi ufike ili apumzike.

“Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano au miaka 10 ni wa kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha kulibadilisha.

“Pili, kazi hii ya urais ni ngumu sana. Kwa hakika nawaonea gere sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi,” alisema Rais Kikwete.

“Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka 10, anaingia mtu mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya.”

Rais Kikwete alisema mfumo huo unamridhisha na hakuna kinachomshawishi abakie madarakani zaidi ya muda wa kikatiba.

“Nina hakika, nchi yetu itapata kiongozi mwingine, bora kuliko hata mimi, kuongoza vizuri nchi yetu,” alisema Rais Kikwete ambaye aligombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995, lakini akashindwa kwenye kura ya maoni ndani ya CCM.

Awali Balozi Onadipe alisema kuwa lingekuwa jambo la maana kwa Afrika kama viongozi wengine wangekuwa na mawazo ya namna hiyo ya kuheshimu Katiba za nchi zao na kung’atuka kwenye uongozi muda wao unapowadia.

Rais Kikwete pia alisema siyo busara kwa kiongozi kuwasikiliza wale wanaoshauri wakisema kuwa akiondoka madarakani nchi itavurugika.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa moyo wa uvumulivu na subira ulonao, ninauhakika ukimaliza muda wako tutakukumbuka, na tutaishia kusema 'afadhali JK'. pindi muheshimiwa 'WAPIGWE TU' atakaposhika dola........ ni shiiiiiiiidar

    ReplyDelete
  2. Pambafu kabisa sasa ulikuwa unagombania uraisi ili iweje? Tatizo la viongozi waafrika sababu kubwa ya kugombea uraisi ni kutaka ulaji siyo kwa ajili ya kulisaidia taifa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad