Siku za nyuma tuliwahi kujadili kuhusu suala la Rwanda kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na athari zake kwa jumuiya, kutokana na tabia ya Wanyarwanda ya kujisikia kwamba wao wamezaliwa kutawala.
Imefahamika kwamba wabunge wa Rwanda katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ndio wamekuwa wakiongoza njama za kutaka kumng'oa Spika Zziwa ili waweze kumuweka mtu atakayepitisha agenda za nchi yao kirahisi.
Mbunge wa Tanzania, Shyrose Bhanji, ambaye aliongoza upinzani dhidi ya kung'olewa kwa Spika hivi sasa amejikuta akiwa adui wa Wanyarwanda kiasi cha kumtungia kashfa ili kumchafua.
Hivi sasa kundi la wabunge wasiomtaka Spika Zziwa wamejipanga kuendeleza njama zao za kumng'oa kwa maelezo kwamba ameshindwa kumchukulia hatua Shyrose.
Kama Watanzania tunapaswa kutambua njama hizi za kumchafua Mtanzania mwenzetu. Huu ni ugomvi mkubwa kuliko wengi wanavyoweza kufikiria.