Pia kuna wabunge wengine walikua wakicheza kwa kufuatisha milio ya miziki iliyokua ikirindima kupitia simu
zao za mkononi. Watu wengi walihamaki kitendo cha wabunge kufurahia Rasimu hiyo hadi kufikia hatua ya kujitoa akili.
Hii hapa siri ya furaha ya Wabunge hao..
RASIMU YA WARIOBA ILIPENDEKEZA:
1. Mbunge akigombea vipindi vitatu basi, awaachie wengine.
2. Mbunge akivurunda ktk utendaji wake, wananchi wana
uwezo wa kumuondoa na kuchangua mwingine.
3. Hakuna mbunge kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, m/kiti wa bodi ya shirika etc. (kwanini vyeo vyote mjilundikie nyie?).
4. Elimu ya mbunge iwe angalau stashahada (diploma) na kuendelea.
RASIMU YA SITTA (ILIYOPITISHWA) IMEPENDEKEZA HIVI:
1. Ukomo wa Ubunge usiwe vipindi vitatu.. Hata wazee waliokaa bungeni miaka 50 kama Kingunge, waendelee tu kugombea. Vijana wanaotaka kuwa viongozi labda wakajaribu kwny SACCOSS sio UBUNGE.
2. Mbunge akivurunda wananchi hawawezi kumfanya kitu chochote hadi miaka mitano iishe na mbunge apewe pensheni yake (Mil.160).
3. Ruksa Mbunge kuwa waziri, Mkuu wa mkoa, DC, Mwenyekiti wa shirika, na vyeo vingine kadri anavyoweza
kujilundikia. Wanaosema mbunge asiwe na vyeo viwili au zaidi, wana "wivu wa kike" (according to Pius Msekwa).
4. Rasimu ya Sitta inasema si lazima mbunge awe na degree, diploma, au cheti. Si lazima mbunge awe na elimu ya sekondari. Si lazima
Mbunge awe amemaliza elimu ya msingi. Hata kama alisoma akaishia darasa la 3 lakini anajua kusoma na
kuandika RUKSA KUGOMBEA UBUNGE.
Sasa je katika mazingira haya wabunge wataacha kukata mauno na kucheza "kitorondo" kwa Rasimu hii kupita?
5. Ongezea kama kuna mengine
JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA
UKWELI...
UPUUZIIII MTUPU....tutakutan kwenye kura.
ReplyDeleteLOADING...
ndiyo maana mengi yanalala hovyo na kutochangia hoja yoyote bungeni, wakija wasomi kama kina Mnyika na Mdee wanawaumbua!!! hoyvoooo!!
ReplyDeleteHii ni ubabe,aibu sana, lakini yana mwisho MUNGU yupo hatutachoka kuomba,atajibu tu.
ReplyDeletestupid idiots.........yani kwa kweli mm natamani ningekua mungu niwaumbue wote siku moja kwa jns wanavyotaka kuendelea kuwaadaa watanzia pumbavu
ReplyDeleteADMN acha umbea hiyo rasimu hata kuingia mitaani kusomwa bado acheni uchochezi
ReplyDeleteTutakutana kwenye Kura mamaeee Kateni viuno tu hukumu yenu yaja.
ReplyDeleteMnachukia nn wakati ndo chama chenu cha majambazi hicho?? Wake up pipo!
ReplyDeleteLabda chama chako wewe wengine hapa nichadema navyama vingine ambavyo si ccm.ccm zamani sio sasa yasasa ni ubatili mtupu.mtu ananenepa mpaka Shingo kama piramidi.unategemea ataleta mabadiliko gani wakati ye mwenyewe kanenepa mpaka ubongo.uchaguzi uje dawa yenu ndogo minyaa tutawatema kama big g.
ReplyDelete