Sitta Akalia Moto, Apambana na Viongozi wa Kikristo

MWENYEKITI  wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, amejiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro mpya dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka wao kuwa ni wa kipuuzi na wa hovyo hovyo.


Huku yeye akisema kuwa waraka wao una lugha ya UKAWA, wao wamesisitiza kwamba ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.

Wakati yeye akikemea waraka wao, maaskofu wamesema ile ilikuwa sauti kutoka mbinguni, na kwamba anapambana na Mungu.

Wakati yeye akisema waraka wao haukuwa na utukufu wowote, wao wamemfananisha yeye na Goliati wa kwenye Biblia aliyeshindwa na Daudi kwa sababu ya jeuri na matusi kwa Mungu. Wamesisitiza kwamba kwa sababu ya jeuri yake, wataanzia pale atakapoishia baada ya Bunge Maalumu la Katiba.

Juzi na jana asubuhi, Sitta alitoa maneno ya kejeli dhidi ya viongozi wa Kikristo, hasa Jukwaa la Wakristo,  ambao walitoa waraka kuonyesha kutoridhishwa kwao na mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akielezea mwenendo wa upigaji kura za kupitisha ibara na sura za rasimu ya katiba inayopendekezwa, akisema amekuwa akituhumiwa kwenye mitandao kwamba anadharau maaskofu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad