Stamina aeleza kwanini remix ya ‘Number 1′ ilihit kuliko remix za nyimbo zingine za Bongo

Msanii wa Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina ametoa sababu ya nyimbo nyingi za bongo zinazofanyiwa remix kutofanya vizuri hapa nyumbani.

Stamina aliitolea mfano remix ya ‘Number One’ ya Diamond na Davido kwa kudai kuwa msanii huyo alijua timing pamoja na thamani ya msanii aliyefanya naye.

“Diamond remix yake ilifanya vizuri kwasababu kwanza nyimbo ilikuwa hit, pili alijua kucheza na timing kitu ambacho ni cha umuhimu sana,” Stamina aliambia Bongo5. “Na tatu jinsi alivyopandisha thamani ya wimbo huo kwa kufanya kolabo na msanii mkubwa Africa kama Davido. Sasa kwanini isifanye vizuri? Kwahiyo timing, yaani muda wa kutoa hiyo remix. Kwasababu hauwezi kutoka remix kabla haijatoka original version. Unakuta original version imekufa wewe unadhani kufanya remix ndo utairudisha? Umefanya nyimbo ya masikitiko, nyimbo ya masikitiko unaifanyiaje remix, unataka usikitike nini zaidi? Remix nyingi zinakuwa ni nyimbo za party au nyimbo za umimi. Yaani zile nyimbo za kama kutuNishiana na kuoneshana nani zaidi. Kwahiyo tatizo kubwa wasanii wengi wanakosa kujua mambo kama hayo,” alisema Stamina.
-Bongo5
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad