Tetesi za Edzen Kuwa Ndani ya Penzi Jipya Baada ya Kutemana na Mkewe Dida
4
October 08, 2014
"Couple" mpya mjini? Mtangazaji maarufu nchini @ezdee255 hivi karibuni ameonekana "benet" na msanii wa filamu na mfanya biashara @mozzah255 Katika mapozi yenye utata. Mtangazaji huyo hivi karibuni aliachana na aliyekuwa mkewe @didashaibu ambaye pia ni mtangazaji wa redio maarufu nchini kwa talaka "chungu" yenye kutawaliwa vyombo vya habari mpaka ikapelekea "Ezdee" kuongelea kwa undani masuala ya ndani ya mkewe na kumshutumu kwenye TV. Hata hivyo mashabiki wengi kwa pande zote hawakupendezwa na shutuma hizo za masuala ya ndoa kuanikwa hadharani namna ile. Mbali na kupiga picha na anayesemekana mpenzi wake mpya wa sasa, "Ezdee" amekana mara nyingi kwamba hawana mahusiano ya kimapenzi. Hata hivyo wengi wamewapongeza kuonesha kuwakubali japokuwa wachache bado wanaona ni mapema sana kujionesha kimapenzi wakati ameacha na mkewe karibuni. Haya sasa....sisi tunauliza, je hawa ni wapenzi au siyo wapenzi?
Tags
Waacheni kila mtu anahaki yakufanya apendacho mradi asivunje sheria
ReplyDeleteMapema kuwa na mpenzi kwani ni msiba?si wameachana tena talaka 3?
ReplyDeleteAU mna mawazo kuwa watarudiana tena?
nakumbuka sakata la taraka yake na dida mdau mmoja alimshauri asiludi kwa wanawake wafanya biashara ili asije akanyanyaswa kwa mambo ya fueza.ni shida. kaludi kulekule penda kulelewa sana huyu jamaa.ukitimuliwa tena usilie.
ReplyDeleteSio penzi jipya hilo, inaelekea tuhuma za Dida zina ukweli ndani yake jamaa alikuwa na spare tyre, haiwezekani muda mfupi tu wawe wamenogeana hivyo.
ReplyDelete