UKAWA Umewafanya Watu Wengi Wasijue Mengi Yaliyomo Kwenye Rasimu

Warioba wakati anawasilisha Taarifa ya Tume Bungeni ali-base sana kwenye Muundo wa Muungano kuliko vitu vingine! Hata takwimu, hatukusikia kuhusu Haki za Binadamu wangapi walisema nini, ila tu kwenye Muungano ndio tulipewa takwimu na Warioba! Ni Warioba ndiye aliyefanya mchakato wa Katiba mpya uonekane kuwa ulilenga tu kubadili Muundo wa Muungano! Kwa bahati mbaya walijitoleza watu waliodaka mrengo wa Warioba na kuufanya ndio main agenda, si wengine bali ni wale waliojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA}! Kiuhalisia huu Umoja ni kwa ajili ya kutetea Muundo wa Serikali 3 tu basi na sio Umoja wa Kutetea Katiba as a whole.

UKAWA mara nyingi wamekuwa wakisisitiza muundo wa Serikali tu bila kuelezea mengine! Wanapodai kuwa maoni ya "Wananchi Walio Wengi" yametupwa mara nyingi yanalenga juu ya Serikali 3, mengine ni ya ziada tu! Na hii imekuwa ni main topic na kwa bahati mbaya vyombo vya habari vingi vimekuwa taken away na msimamo huo.

Matokeo yake ni kwamba mambo mengine mengi yaliyomo kwenye Rasimu watu hawatayajua na tunaweza ikifika Aprili, 2015 tukajikuta tunapiga kura juu ya Muundo wa Muungano, only that.

Ni wakati sasa wa kubadili mtazamo wa kiu-UKAWA na kuangalia kila kitu kilichomo kwenye Rasimu na kufanya maamuzi sahihi! Tuachane na wenye maslahi binafsi juu ya Muundo wa Muungano.
Tujadili zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad