Watz saluti kwa kushika mabango.....ila ninamaswali machache...
Ivi Miss Tanzania ina faida gani kwa Maisha ya Watanzania Masikini wenye Taifa Tajiri ambalo hata rais wake hajui ni kwanini wananchi wake ni masikini???
Ivi umejaribu kufikiri Miss Tanzania inasaidiaje Kuboresha maisha yako na ya watanzania masikini walio wengi tena walioko vijijini???
Miss tz inaboreshaje huduma za Afya ili kupunguza vifo vya wanawake, watoto na watanzania masikini wenye nchi Tajiri???
Miss tz inaboreshaje Elimu nchini hasa shule za Umma ambazo wengi wanaosoma huko ni watoto wetu sisi watanzania masikini wenye Tanzania Iliyojaa Utajiri????
Miss Tz inaboreshaje huduma ya maji nchini wakina mama wengi tunabakwa kwa kufuata maji umbali mrefu???
Hii nguvu inayotumika kwa miss tz, kwa nini tusiihamishie kwenye mustabakali wa maisha yetu ya sasa na ya baadae yaani vizazi vijavyo kwenye Katiba pendekezwa???
"Katiba pendekezwa" umewahi kuifuatilia hata kwa dk 1??? Unajua kama ndo imebeba maisha yako, wajukuu wako, vitukuu na vilebwe??? Una mchango gani katika kupata Katiba Bora ya nchi yetu! umeshajiuliza na kutafakari???
Tuache kutumia fikra zetu kwenye vitu visivyo vya msingi katika maisha ya watanzania tulio wengi.... samahani lakini
Miss tz fanya yako mama...pole kwa yalokukuta.. waandaaji Wamekupa taji wenyewe kwa sababu zao wenyewe, so wasikusumbue..tena wakuache kabisa Mwanamkelive wangu, ningekuwa mimi ni wewe nisingeenda kwenye press ya kujichoresha...dhambi hii abebe Mratibu wa mashindando na team yake...
Watz tulio wengi ni Wajinga sanaaa hasa katika kuchekecha masuala yapi ya Msingi na yapi ya yasiyo ya Muhimu! na si kosa letu bali ni mikakati ya watawala wetu kuhakikisha wananchi tunajikita kuongelea Mambo ambayo hayana Msingi sana kwa wananchi wengi, badala ya kufuatilia masuala ya msingi yanayohusu hatma zetu... na wamefaulu katika hilo na wataendelea kufaulu kwa sababu ubora wa Elimu yetu inazidi kuporomoka...usitegemee mtz aanze kuongelea mfano uchakachuaji wa Katiba Pendekezwa, wala kuhoji huduma muhimu zinazotokana na kodi yake.. never!!!
Mfano rahisi angalia kwenye mitandao ya kijamii ya watanzania na ulinganishe na nchi zingine mambo wanayoyapa kipaumbele katika kuyajadili kwa nguvu kama hii tuliyoweka kwa Miss Tz...Ukilinganisha Nguvu inayotumika kwenye Katiba Pendekezwa na Nguvu ya Miss Tz kuna tofauti kubwa sana...
Pia Angalia magazeti yanayosomwa sana, kisha utawajua watz tulio wengi.. si wote.. utatujua tuliowengi ni watu wa aina gani....
Waandishi wenzangu watendeeni Haki watanzania masikini ambao Taifa lao ni Taifa Tajiri sana lakini ndo Taifa lenye watu masikini sana...waandishi ndo maana tunaitwa makanjanja!! Ivi kweli airtime na rasilimali kubwa hivi mkaziweka kwa nguvu yote hii in the name of Miss Tz???? Ebu tuwahurumie Watz na sisi wenyewe na Taifa letu hili..... sisemi kama msiandike ila mmeshupalia sana kana kwamba Miss Tz ni "Katiba pendekezwa"
~Joyce Kiria
We house maid hebu tulia.Watu wasiongelee jingine sababu ya katiba mpya?Kila jambo na wakati wake.Na hii ni wakeup call,wabongo sasa hivi hawapelekwipelekwi tu.Taji avae anayestahili.
ReplyDeleteWe Joyce peleka kengeza lako huko.hlf ukasome maana unakurupukaga kama jengo limeshika Moto.kilakitu nawakati wake katiba hatuna deal nayo hio katiba niyawatu wachache wanayoipendekeza ipite kwa mabavu kwa faidazao.hakuna kitu chakutufurahisha kwenye hio katiba hatuitaki nahatuwezi kuiongelea tutakutana kwenye uchaguz ndo watakapotujua watanzania wasasa tupoje.nakingine we mwanamke unakiherehere nakichwani kwako ni empty.kafue nachupi za sitti umpigie Pasi unajikombaga sana kwawatu.hatumtaki miss tz natutasema ndio kwani tz siyetu?akagombee umalaya huko apewe taji hili sio lake kapendelewa
ReplyDeleteOOO KAZI KWELI KWELI!!! MISS MTEMVU RUDISHA TAJI SIO HALALI YAKO JAMANI
ReplyDeletekatiba wewe unailipia nini?miss tanzania tulipia kiingilio mazafanta
ReplyDeleteJoyce poyoyo unatafutaga kik kinguvu kajambe kuleee,nenda shule kwanza Utanue wigo wakichwa chako.unakurupuka tuu
ReplyDeleteunadhani ukisema katiba ndio tutaacha kusema ukweli? mseme na sitti kwamba kadanganya umri wake ni upi ? kwenye mashindano alisema ana miaka 18 kwanye mahojiano na waandishi wa habari kasema ana miaka 23 kwenye passport yake na leseni ya udereva ni miaka 25. Please Sitti tuambie miaka yako sahihi ni mingapi Tena useme kwa kumwogopa Mungu. Nasikia siku uliyoshinda ulienda kwa nabii flora kushukuru Mungu, Je ni mungu gani huyo??? kwa ushauri wa bure miye naona urudishe hilo Taji maana dhamira yako inakuwa inakuhukumu kila siku kuwa sio haki yako!!!!
ReplyDeletemwakilishi wa wananchi wa temeke msaidie huyu binti kumwambia umri wake sahihi!!!au nawe hujui??
ReplyDeletehee bado umengangania hilo taji???
ReplyDeleteSASA KWENYE MISS WORLD UTAENDAJE JAMANI ??? MAANA WAMESHAJUA KUWA UMEFOJI MIAKA??
ReplyDelete