Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake wanaopingana na msimamo wa chama hicho kuhusu katiba inayopendekezwa kurudisha kadi na kuondoka mara moja ndani ya chama hicho.
Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake wanaopingana na msimamo wa chama hicho kuhusu katiba inayopendekezwa kurudisha kadi na kuondoka mara moja ndani ya chama hicho, badala ya kutumia mgongo ya CCM kuwapotosha watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati kuu wa halmashauri kuu ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mh Stephen Wassira, muda mfupi baada ya kupokelewa na wawakilishi wa wananchi wa mkoa wa Mara, ikiwa ni siku chache tu baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba, ambapo amesema kuna baadhi ya wana CCM wamekuwa wakitumia mgongo wa chama hicho kuwapotosha wananchi kuhusu katiba hiyo inayopendekezwa.
Hata hivyo Mh. Wassira ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu, amesema katiba inayopendekezwa endapo itapitishwa na wananchi itajibu kilio cha miaka mingi kuhusu ukiukwaji wa maadili vikiwemo vitendo vya rushwa ndani ya jamiii.
katika "collective responsibilliyt" ambaye anapingana na msimamo wa wenzake kwa chama cho chote ni utaratibu tu ahame hakuna haja ya kupinda migongoni mwa wenzako na kudai angalia nilivyo mrefu simama peke yako kama una hoja itapimwa acha kuwa fisi asiye na msimamo ni UNAFIKI
ReplyDeleteHawa CCM wamezoea kujiona km Miungu watu,wanachofanya,wanachoamua ndoio kiwe hicho hicho kisibadilike km QUR AN tukufu,kila kitu kina mwisho wake....Mwenyezi Mungu anasema "KULL MAN ALAIHA FAN" (kila kitu kina mwisho wake)....na nyinyi CCM tumieni nguvu zenu zote lkn ipo siku yenuuuu.....Mmetuchoshaaa hasaa kwa kweli,hamna kimoja cha maana mnachotufanyia....
ReplyDelete