Takriban watu 28 wameuawa na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab waliovamia basi la abiria jijini Nairobi, Kenya.
Tukio hilo limetokea alfajiri leo saa 11:30 kwenye eneo la Mandera.
Kamishna Msaidizi wa kaunti ya Mandera East, Elvis Korir alisema taarifa za awali zimedai kuwa wanamgambo hao takriban 100 waliisimamisha basi hiyo na kuamuru watu wote watoke nje.
Anadai kuwa abiria hao waliwekwa kwenye makundi mawili ya Wasomali na wasio wasomali. Alisema kundi la wasio wasomali walimiminiwa risasi.
Abiria 59 walikuwa wamepanda basi hilo.
Chanzo: Daily Nation
Al-Shabaab Wavamia Basi na Kuua Watu 28, Nairobi
November 23, 2014