Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, mwanadada Faiza Ally ameamua kuwatolea uvivu watu wanaodai kuwa ameachwa na mheshimiwa huyo kutokana na mavazi yake.
Faiza ambae ana mtoto na Sugu, katika instagram ameandika:
“Sasa leo ngoja nifunguke…. Yaani nikiweka picha zangu kwa raha zangu mnaanza kusema oh ndio maana SUGU kakimbia ndio maana kaniacha Nasema hivi MIMI NDIO NIMEMUACHA mkome kunisema nimeachana na nimemuacha tukiwa kwenye process za ndoa na tulishakutana na padri na kwenye jumuiya nilisha anza …..
Kuna vitu vikinifanya niondoke kabla ya ndoa ambavyo vitabaki kuwa vya kifamilia ……. Nyie mna muona sugu Kama si mtu wa kawaida mm namuona Kama alie kuwa mpenzi wangu na Sasa ni baba wa mtoto wangu …. Lkn anajua ubora wangu na faida zangu Pumbavu zenu nyote mnao zani niliachwa tena kwa mavazi anajua na anapenda mavazi yangu ….. Nachukia kuamka asubuhi na kukuta comments za kusemwa vibaya…. Nyie mnajua tabia zake ????? Au mnamuona kwa mbali ?????”
Aliyekuwa Mke wa Muheshimiwa Sugu Afyatua Matusi Mtandaoni
November 26, 2014
Tags