Baba Diamond Amsaka Wema Sepetu, Ataka Kujua Kisa cha Kuachana

Stori: Musa Mateja na Gladness Mallya

Baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ kummwaga mwanaye, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baba mzazi wa jamaa huyo, Abdul Jumaa ‘Baba Diamond’, amenaswa akimsaka mrembo huyo ili kujua mbichi na mbivu.

‘UBUYU’ KUTOKA KWA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya kusikia habari za mwanaye kumwagwa na Wema aliumia roho kwani anamkubali Wema kuliko warembo wengine wote ambao walishatembea na mwanaye huyo.

“Hakuna habari mbaya kwa baba Diamond katika kipindi hiki kama ishu ya Wema kumwaga.

MAUMIVU
“Unaambiwa ‘mdingi’ aliumia sana kwani huwa anampenda mkwe wake Wema.
“Baba Diamond anaamini kabisa kwamba Wema ana nyota ndiyo maana Diamond akiwa naye huwa anang’ara sana,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
TATIZO NI NINI?
“Amekuwa akimsaka Wema ili ajue tatizo ni nini na kama kuna uwezekano wakae wayamalize.”
Habari zilieleza kwamba, kwa wiki nzima, baba Diamond amekuwa akimfuata Wema nyumbani kwake, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar lakini amekuwa akimkosa.

RISASI JUMAMOSI MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili (Risasi Jumamosi) lilipiga kambi kwa siku kadhaa getini kwa Wema huku likiweka mtego ambao juzikati ulimnasa mzee huyo.Baba Diamond alishuhudiwa akigonga geti kwenye nyumba hiyo anayoishi mkwe wake na kuzungumza na mlinzi ambaye alimwambia kuwa mwanadada huyo hayupo.

Kwa mujibu wa mlinzi wa getini hapo mzee huyo alikuwa akiomba kumuona Wema ili amuulize sababu ya kumwacha Diamond ambaye walikuwa na mapenzi kama ya njiwa.Baada ya kumkosa mzee huyo alisema anaendelea kumsaka hadi atakapompata ili wazungumzie ishu hiyo kiundani.

WAZO LA KWENDA KWA DIAMOND
Baada ya kuondoka nyumbani hapo kwa Wema, mzee huyo alisema huenda yupo kwa Diamond na hata kama hatakuwepo itabidi azungumze naye juu ya ishu hiyo ya kuachwa na Wema.
Ilisemekana kwamba mzee huyo anafanya jitihada zote hizo kwani kwa upande wake Wema ndiye mwanamke pekee anayemkubali.

Ilielezwa kwamba baba Diamond anataka kuwasikiliza kila mmoja na kuhakikisha anawaunganisha upya ili waendelee na safari yao ya kimapenzi hadi watakapooana.

TUJIUNGE NYUMBANI KWA DIAMOND
Huku wanahabari wetu wakipeana ishara kuwa wawahi getini kwa Diamond au Dangote, walipofika mahali hapo, dakika chache baadaye mzee huyo alinaswa getini kwa mwanaye maeneo ya Sinza-Mori, Dar akigonga mlango.

GETI LAFUNGULIWA
Baada ya kugonga kwa muda mrefu huku akiwa amefura, alitokea msichana ambaye alimfungulia mlango mdogo wa getini ambapo alikuwa akizungumza naye akiomba kuonana na Diamond bila mafanikio.

MAMA DIAMOND KWA MBALI
Wakati mzee huyo akiomba kuingia ndani, kwa mbali alionekana mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kwa mbali akiwa amekaa barazani bila kutambua sauti ya baba Diamond aliyekuwa akizungumza nje ya geti.

MADANSA WA DIAMOND
Hata hivyo, baadhi ya madansa wa Diamond walikuwa wakiingia na kutoka bila kumjali mzee huyo huku mmojawao akimfananisha bila kuwa na uhakika.Baba Diamond alipoona imeshindikana kumuona mwanaye huku mlango ukifungwa, aliondoka kwa huzuni akiamini ipo siku atawakutanisha Wema na Diamond ili kumaliza tofauti zao.

Gazeti hili liliwatafuta zilipendwa hao kwa nyakati tofauti lakini hawakupatikana hivyo jitihada za kuwafikia zinaendelea au hata wao wenyewe wakisoma habari hii watatupigia simu zetu kwani wanazo namba.

TULIKOTOKA
Huko nyuma, Diamond aliwahi kudai kwamba baba yake alimtelekeza yeye na mama yake ambapo waliishi maisha ya tabu na kushindwa kusoma kwa kukosa ada lakini hivi karibuni alitangaza kumsamehe.

Wakati Diamond akifanya kufuru kila kukicha na kugawa magari, baba yake anaishi peke yake,  maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar.
Credits:Global Publishers

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. waswahili kwa chuki hatariiii hahaha yote ayo magazeti ya udaku kuwazushia story kumbe ni hizo gari 2 tu oohhh 3 nimesahau na ile ya marehemu gurumo lol ajab alivompa marehemu mlifurahia na kumpongeza sasa amempa mama ake kipenzi na mpenzi wake imekuwa mgawa magari binadamu kazi kweli kweli (sisemei mzee wake mana hayanihusu) ila magazeti kama hamtumwi na wahusika wenyewe basi mna chuki binafsi mana hii ni zaid ya uwandishi tuacheni ushamba watz jamani mjue tunatia aibu jirani apo wakituona!!

    ReplyDelete
  2. hawa mababa wasio jua umuhimu wa kumraise mtoto na kumuhudumia leo unaanza kujipendekeza ni upuuzi kabisa, mimi ni baba pia na nina watoto, najitahidi kuwaraise kadri niwezavyo, sasa huyu jamaaa limetelekeza huyu dogo asingefight akasimama mwenyewe angesanda, pia hata [pengine aangekufa kwa kukosa huduma bora za afya na mengineyo, jifunzeni wababa wenzangu mtunze mtoto wako na mpende.. Maisha ni safari ndefu, ila usitegemee sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad