Breaking: JAJA Ajiondoa Rasmi Yanga, EMERSON Achukua Nafasi Yake

MSHAMBULIAJI Genilson Santana Santos ‘Jaja’ amejiondoa Yanga SC
akiwa likizo nchini mwao, Brazil na sasa nafasi yake itazibwa na
kiungo mkabaji, Emerson Oliveira Neves Roque, Jaja amesema ana matatizo ya kifamilia yanayomzuia kurejea
Tanzania kufanya kazi.
Emerson mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Rio de Janeiro,
anakuja Yanga SC akitokea klabu ya Bonsucesso ya mjini humo, ambayo imewahi kucheza Ligi ya Serie B
mara mbili, ingawa kwa sasa inacheza ligi ya jimbo la Rio.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumanne kwa ajili
ya kufanyiwa majaribio na akifuzu atafanyiwa vipimo vya afya, kabla
ya kusajiliwa. Wazi mchezaji huyo ana nafasi ya kusajiliwa Yanga SC
kwa kuwa analetwa na kocha Maximo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad