Ripoti ya BUNGE kupitia Kamati ya PAC sasa inakataliwa kutokana na maslahi ya CHAMA, Chama kimekuwa pango kuu la wezi na hivyo kwa maneno ya Warioba CCM Maslahi. CCM imani imebaki kwa Butiku na wenzake pekee.
Kitendo cha Nagu kusema kuita watu wezi sio vizuri bila kusema kama kuiba ni vizuri ni dhahiri kuwa CCM haina kinyaa tena na wezi, mafisadi wala watu wenye tabia za kutowajibika ktk kazi kama Pinda.
CCM imeshindwa kutetea umma na hivyo kutetea maslahi yake na wanachama wake viongozi pekee huku wanachama wadogo wakiachwa kuishi kwa bahatisha za maisha.
Maneno ya Kibajaji kuwa kumpatia mtu hela haliwezi kuwa kosa, ni kuthibitisha kukosa kwa maadili ndani ya chama mchana kweupe, mtumishi wa umma anapatiwa fedha na mtoa huduma za jamii kwa mikataba ambayo kila siku inabishaniwa kuwa ni ya wiz wizi. Haingii akili mwa mtanzania isipokuwa mwanaccm tu kuwa waziri wa nishati wastaafu na aliopo wapate chochote, ag mstaafu na aliyepo atape chochote, mawaziri kama tibaijuka apate chochote, watumishi wa umma na wengine wa TRA wapate chochote kutoka kwa mtu mmoja bila kujua hela hiyo ni hongo kwa namna fulani. mbona hajagawia watu tu mitaaani? ni wazi wamepewa hela kwa nyazifa zao. na ni rushwa.
Rais yuko kimya, na uozo huu. Serrikali inadai hela ni za mtu binafsi, je iweje ag na cag watoe maelekezo ya kutoa na kukagua fedha za mtu binafsi??? JK tujibu hilo.
Tukishindwa kwa hili basi jamii ya tanzania bila kujali hasara na mwelekeo wa mbele, inapaswa tukatae kwa nguvu zote watu wa namna hii wizi wa namna hii, na matumizi mabaya ya ofisi.
Nawasilisha