Na Imelda Mtema
MTANGAZAJI mwenye maneno lukuki kutoka Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amesema kuwa endapo mtalaka wake, Ezden Jumanne akitaka kuoa yeye atakuwa wa kwanza kutoa mchango wa harusi hiyo.
Dida ambaye kwa sasa yupo singo, alisema japokuwa wameacha na Ezden, lakini hana bifu naye kwa sababu anaamini kuwa yuko katika harakati za kutafuta mke bora hivyo haoni shida kumchangia.
“Ninachoamini mimi Ezden bado anasaka mke mwema na hiyo ni nzuri na wala siwezi kuwa na bifu na mtu wake yeyote atakayempata, nitapenda sana. Haya ndiyo maisha yasiyokuwa na chuki yanayotakiwa,” alisema Dida.
Dida Afunguka Kuhusu Ezden Kuoa Mke Mwingine Baada ya Wao Kuachana
November 27, 2014
Tags