Taarifa zilizosambaa ni kwamba Wema na Diamond wanatarajiwa kwenda Uganda December, lakini kila mmoja akiwa na mwaliko wa mwenyeji tofauti. Diamond atakuwa mgeni kwenye show ya Zari The boss lady, huku Wema atakuwa mgeni wa show ya Jose Chameleone.
Maswali ya uhusiano wa staa wa filamu Wema Sepetu pamoja na staa wa muziki Diamond Platnumz yamezidi kuongezeka kama kweli wameachana ama laa, baada ya wote wawili kujihusisha kupigia debe show hizo mbili tofauti zinazotarajiwa kufanyika siku moja, mwezi mmoja, jiji moja lakini kumbi tofauti.
Diamond ambaye amekana kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Zari, amepigia debe show ya ‘Zari All White Ciroc Party’ huku akitarajiwa kuwa mgeni kwenye show hiyo. Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii ameandika:
“kama mlivyokuwa kimya wakati nasupport watu wengine… Muendelee hivyohivyo…Hasa niwaskie kwenye hii #AllWhiteParty 18th Dec 2014 at Guvnor night club in Kampala UG Usikose!… @zarithebosslady”
Huku Wema naye amepigia debe show ya Jose Chameleone ‘1 Man, 1 Show, 1 Million’ huku akiahidi kwenda Uganda kuhudhuria show hiyo, ameandika:
“Hatari….!!!! Hatari….!!!! Hatari….!!!!! Sijawahi kufika Uganda lakini kwa hii ntapanda ndege kabisa kwenda kumsupport my brother @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone @jchameleone …. Basi tutakutana pale kati tar 18 kwenye hio show ya kufunga mwaka… Ama nene….”
Show zote mbili ya Zari na ya Chameleone zinatarajiwa kufanyika Kampala siku moja ya Dec.18.
Drama: Wema kuhudhuria show ya Chameleone, Diamond kuwa mgeni wa show ya Zari, zote kufanyika siku 1
November 27, 2014
Tags