Gardner G Habash ‘Kapteini’ Adaiwa Kumpandisha Lady Jay Dee Kortini

Na Musa Mateja
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.

Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.

Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.

“Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali.

“Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane kiroho safi lakini Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani anaogopa ule usemi kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria.”

Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, kitendo cha Jaydee kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.

Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na kuamua kukimbilia mahakamani. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: “Kaka kusema kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata wapi dah.”

Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aitwaye Wakazi.
GPL
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ILA gadner wewe mbona unauwezo wakupigakazi naukapatachako ukawa namaisha mazuri ukafurahi tu.jamani acheni kupenda wanawake wenyevitu,unampenda mwanamke anakazi nzuri au biashara nzuri kwahio umefata mteremko?haya wewe mwanaume unanini chahasa mpaka upende waliotayari km nimtwangio wapo kibao wenyenayo nainakita vema tu.mwishowe mnazalilika maana wanawake wasasa mnawajua ukimzingua kidogo Yuko resi mbaya najeuri ya pesa.ifike wakati ukimpenda mwanamke tayari Yuko njema make sure nawewe uko njema pia muende sawa lakini huna kama ezden halafu unajipandisha mabega utajidharaulisha tu maana wanawake wasasa sio wazamani.penda cha size yako mwanamke ye akimpenda mwanaume mwenyepesa nisawa yeye ni mwanamke nandivyo ilivyo sasa mmeigeuza kwenu wanaume mtadhalilika sana.sabbu hata hao wenyepesa wanaume wanadhalilisha wanawake sana tu so hatananyie wanaume wapenda slope mkidhalilishwa nisawa tu ngoma droo.mmefundisha wanawake tabia mbaya naukatili acha yawakute.

    ReplyDelete
  2. HA HA HA KWELI AIBU YA KUFUNGA MWAKA.NIMEAMIN MUME SI NDUGU YAKO KUMANINA

    ReplyDelete
  3. GADNER USIKUBALI MPELEKE HUYU MKOMAVU MAHAKAMANI MGAWANE MALI ILA HUYO DEMU WAKO VESTINER SIO SAHIZI YAKO NI MTOTO MDOGO SANA KWAKO, YULE DEMU WAKO MAGIE YUPO WAPI? ALIKUWA MZURI SANA, MSHITAKI HUYO DEMU KAPOTEZA NGUVU ZAKO BURE UNA MTOMBA KILA SIKU ALAFU HAPATI MTOTO HAONI KAMA KAKUPOTEZEA MUDA? KAMA NI WATOTO MNGEKUWA NAO WANGAPI TANGU UANZE KUISHI NAYE? USIMSAMEHE HUYO

    ReplyDelete
  4. JIDE KATOBWA WW MTOT AZAI PIGA CHINI FASTA UYO BIB ETI BINTI MACHOZI NDO MAAN ALIKUWA ANAMTAKA MWINYI

    ReplyDelete
  5. unajua watu washenzi sana achen ujinga kama azai zaa wewe yeye mungu ajampa kwan wangap hawajajaliwa kupata mtoto wanaish nyie mnaongea tu alizoea kulelewa kajiachia tafuta vyako we simwanaume mshenz uyo kaka subir nawewe yatakukuta kama siwewe mwanao au mjukuu wako hatopata mtoto mnaropoka tu ustupd huo kama huwez ongea au kuchangia vyamsing acha kwan lazima

    ReplyDelete
  6. Acheni ya watu angalieni yenu wabongo bwana.....hili ni moja wapo ya sababu zinazo tufanya tunadharauliwa hata na wageni tunaendekeza sana mambo ya watu wengine badala ya kufanya kazi za maana .. aya semeni ndiyo imeisha kuwa ivyo.

    ReplyDelete
  7. Haki sawa kwan pia jamaa anamchango mkubwa sana had jd kafika pale kwani alikua hawez kujimanage so its better to fight 4 justice kama wasemavo haki sawa

    ReplyDelete
  8. Gadna aachane na pesa za mwanamke!afanye kazi apate pesa zake!mwanaume utategemeaje pesa za demu bana?!ni aibu tupu

    ReplyDelete
  9. Ndo maana aliimbwa "Wanaume kama mabinti", Bojo Mshaija!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad