Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.
Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.
Hukumu ya Mahakama ni ya halali na haina utata na Zitto wala CAG wala TAKUKURU hawajaonesha kuwa ilikuwa ni batili au ya kughushi.
Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.
Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho ni hii na hapa wamepata mwanya.
Nnasikitika kusema na nnaliona linakuja la Serikali kuingia gharama kubwa ya kulipa zaidi ya mara mbili au tatu hizi fedha ikiwa watafata akili za akina Zitto.
Nnashauri, wajadili hili suala bungeni lakini shauri liwachwe kesi kumi zilizopo mahakamani zinazoihusu IPTL zikamilike.
Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.
Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata kesho na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.
Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri leo, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.
By FaizaFoxy