Halima Kimwana Akana Kuhusika na Uhusiano wa Diamond na Zari
0Udaku SpecialNovember 20, 2014
Mdada wa mjini ambaye ni dada wa hiyari wa msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Halima Kimwana amedai kuwa hahusiki na uhusiano unaoendelea kati ya kaka yake huyo na mrembo kutoka Uganda, Zari. Akizungumza na waandishi wetu, Halima alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala lolote la Diamond na uhusiano wake na Zari kwa kuwa hahusiki na jambo lolote kati yao. “Jamani mimi sifahamu chochote na siwezi kuzungumzia kwa kuwa sijui na sihusiki,” alisema Halima anayedaiwa kumuunganishia Diamond kwa mademu kibao japo tuhuma hizo anazipinga.