Baada ya Spika wa Bunge kuahirisha Bunge mara mbili siku ya leo Novemba 29 ili kuipa nafasi kamati ya PAC iweze kufanya marekebisho ya maneno yaliyoandikwa kwenye maazimio yaliyowasilishwa na Kamati ya PAC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zitto Kabwe ametaja majina ya walioteuliwa na Kamati hiyo kuandika maazimio ya kuwajibisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook (@Zitto Kabwe) ameandika majina ya wajumbe hao.