Imegundulika Kumbe Mastaa wa Kike Bongo Hujiuza Kupitia Mitandao ya Kijamii

MWANADADA mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameibuka na kueleza kwamba mastaa wamegundua njia mpya ya kujiuza ambayo ni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akistorisha na gazeti hili, Aunt Lulu alisema mastaa wengi wa kike wanajiuza kwenye mitandao ambapo mapedeshee waliopo mikoa mbalimbali wakishaziona picha zao huwa wanawatafuta kwa udi na uvumba ambapo wanawapigia simu na kuwatumia fedha na tiketi za ndege ya kwenda na kurudi.

“Yaani mastaa wa kike hatulali unakuta pedeshee anakutumia tiketi ya ndege unamfuata mkoani ukienda usiku asubuhi umesharudi Dar unaendelea na mambo yako ndiyo maana unawaona wasanii wengi wa kike wana fedha lakini kazi wanazozifanya huzioni,” alisema Aunt Lulu.
GPL

Top Post Ad

Below Post Ad