Jee, kitendo cha ITV Kuendelea Kumpa Airtime Jaji Warioba Sio uchochezi Katiba Mpya Ikataliwe?

Namsikiliza kwa makini sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akiizungumzia mchakato wa kuipigia kura ya maoni, ama kuipitisha katiba pendekezwa au kuikataa.

Kwa vile baadhi ya maoni ya Tume ya Warioba, yalipigwa chini, it is obvious Jaji Warioba, atakuwa ni mpinzani number 1 wa katiba pendekezwa, kwa kupuuza maoni ya wananchi, yaliyopendekezwa na Tume yake.

Kwa vile baada tuu ya kuwasilisha rasmi ile rasimu ya Tume ya Kukusanya Maoni, kwenye Bunge Maalum la Katiba, Tume ya Warioba, ilivunjwa rasmi!, hivyo as of now, Jaji Warioba, sio authority tena katika mchakato huu wa katiba mpya!, bali ni mwananchi tuu wa kawaida, mwenye uhuru wa kutoa maoni yake kama mwananchi mwingine yoyote!. 

Jee, kitendo cha ITV kuendelea kumpa airtime Jaji Warioba, huu sio uchochezi wa kupigia chapuo Katiba Pendekezwa, ikataliwe?!.

Anachokifanya Jaji Warioba ni kuwaelimisha Watanzania, kuielewa katiba pendekezwa imekosa nini, hali inayoweza kupelekea katiba mpya kukataliwa!, sasa inachokifanya ITV, ni kuwasaidia Wananchi kuielewa Katiba Pendekezwa, hivyo kuwachagiza kuikataa, jee huu ni ukombozi kwa Watanzania au ni uchochezi?!. 

Kwa vile Tume ya Warioba iliisha vunjwa kitambo, kwa nini ITV inaendelea kumkumbatia Jaji Warioba, kwa kumpatia airtime kubwa namna hii, badala ya airtime hii kupatia Andrew Chenge na Samuel Sitta ili wainadi Katiba Mpya?!.

Jee ITV ni wachochezi au wakombozi?!.

Kwa vile mmiliki wa ITV ni Mzee wetu, Mhe. sana, Dr. Reginald Mengi, kama ITV ni Wachochezi, inawezekana pia ikawa mchochezi mkuu ni mzee wetu huyu?!, na ikiwa ITV ni wakombozi, jee inawezekana Mzee wetu huyu ni Mkombozi?!.

Wasalaam.

Pasco.
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna Tatizo hata kidogo,Ni muhm kuzidi kuwaelimisha wananchi wapate kujua faida na athari ya kila kipengele kilichomo ndani ya KATIBA iliyopitishwa na BUNGE la jamhuri ya MUUNGANO,Tanzania hatutoweza kuendelea bila mabadiliko....MABADILIKO LAZIMA.

    ReplyDelete
  2. Ulaghai mwisho wake 2015, mtasoma nyekuuundu au kundu ipi ni kundu, maeee

    ReplyDelete
  3. Kuna tatizo gani kwani tukielimishwa kuhusu katiba pendekezwa? arent we supposed to know what's in our constitution? Naipenda CCM lakini kila siku wazidi kunidisapoint wamekua kama mwana mtukutu and soon to be dishonoured!

    ReplyDelete
  4. jamani ndugu zangu embu tuelewe ukweli katiba in hatua kuu tatu ya kwanza kukusanya maoni, ya pili bunge la katiba na ya tatu kura za maoni nisichoelewa mimi ni kuwa kama maoni ya tume ya jaji Warioba ni sahihi na hayakutakiwa kujadiliwa na kupigiwa kura na bunge la katiba ni kwa nini tuingie gharama za kuwa na bunge hilo?je ni ukweli kuwa wabunge wote walitakiwa kukubbaliana na kila kitu kilichopendekezwa na tume?kama ndio hatukuwa na haja ya kuwa na hilo bunge swala la msingi kwanini Jaji Warioba ana amini kila kilichopendekezwa naye kilikuwa sahihi?je kama ana amin katika misingi ya demokrasia na ukweli kwanini asikubaliane na yaliyotokea bungeni?kwangu binafsi nafikiri kuna haja ya watu kupata elimu zaidi kuhusu kazi na malengo ya taasisi zote tatu za mchakato wa katiba sababu hata hao ukawa kama wanaamin katika demokrasia ambayo wanaipigania kila siku wasingetoka bungeni sababu demokrasia ni mfumo wa kiunwana na unakufanya ukuabliane na kutofutiana kwa mitizamo na wenzio! inakulazimu kukubali pale wenzio wanapokushinda kwa hoja na nguvu y a kura.

    ReplyDelete
  5. bado ninaendelea ndugu zangu kama , tuliwasikia hawa UKAWA wakijinadi kuwa wapo kwa ajili ya kutetea katiba ya wananchi lakini mkutano waliofanya jangwani ni kuwa wanaungwana kwa ajili ya uchaguzi mimi Napata kigugumizi cjui kama kweli hawa watu walikuwa na nia ya kutupatia katiba mya ama wanatatfuta political profile ya kufullfill dreams zao za kwenda ikulu! kwa maana hiyo wanachi wenzangu tufikie mahali tuwaelewe wanasiasa wetu wasitufanye punda wa kufikia malengo yao! tuingoje katiba tuisome tuipigie kura kwa utashi wetu bila kushawishiwa na hawa wasaka tonge!

    ReplyDelete
  6. We kichaa hapo juu kapatedozi.naona unarudi nyuma kama mwanga.ukawa hawazungumzii katiba walishaikataa toka mwanzo kwani ulikuwa kipofu hukuona mavi wewe.ccm wameipitisha kwamabavu ulitaka waongee halafu mseme wanafujo.afanyacho warioba ni sawa kabisa siomnapigia Kura hii katiba bilaluilewa itawacost.msome muielewe.kwann upandemmoja tu uikazanie wengine wakatae?hatapicha hamuoni?ukawa wao wameamua kutokuizungumzia hawaitaki badalayake kujikita kwenye uchaguzi nakufanya Yao sasa wepoyoyo hapo juu uelewe Hilo.na2015 waliokaa ubunge miaka 20 ambao siwachapakazi kaziyao kujamba tu nakusinzia bungeni mjue hampiti tunawajua tutawafanyiakazi tutawafyeka kiroho mbaya wachapakazi wanajulikana wale wengine nyie hongeni tutakula nahatuwachagui mmejisahau sana bungeni,acha tuwawajibishe tutawafyeka pyeeeee subiri.nawapinzani lazima tutawajaza maana nyie mmejisahau.

    ReplyDelete
  7. ww msenge kweli kwaiyo unataka warioba apigie promo kitu kibovu aache kizuri......fala mkubwa ww na mtapotezewa sana na mtaomba poo nyie wasenge na iyo katiba yenu ya kisenge mliopendekeza na wake zenu lakini cio ya wananchi

    ReplyDelete
  8. Anonymous hapo juu hata lugha unayotumia inaelezea wew ni mtu wa namna gani ! ukweli utabaki pale wenye busara watapima ila kwa muundo wa nchi yetu ni ngumu sana kwenda ikulu kwa kutumia violence hawatafanikiwa hatuhitaji hvyo watu wasijifanye manabii kwenda shetani ana afadhali yao! sudhani kama hiyo UKAWA ina suluhu ya matatizo yetu hata walichotofautiana kule bungeni hakikuwa maslahi ya wananchi ilikuwa ni muundo wa serikali ambayo kwa asilimia kubwa ni maslahi ya viongozi wew ulisikia UKAWA wakitoka bungeni kwasababu ya sera za kilimo au mifugo ? ndugu yangu tumia akili uliozaliwa nayo ni zawadi kutoka kwa mungu usikubali mtu ageuze kichwa chako sterling ya gari! Fikiria ndugu yangu hawa wanasiaisa alivyo vichwa kuvimba tu badala ya kwenye katiba waeke sera za kuwawezesha wajasiriamali wao wanahangaika na kutafutia vijana ajira jiulize lipi bora kuwawezesha vijana wajiajiri au kuwaleta wazungu hapa wawekeze alafu waajiri vijana wetu! haya yalikuwa ni mambo ya msingi kwenye katiba hata Mzee wetu Jaji warioba alipashwa kulifanyia kazi hili na sio kukimbilia muundo wa serikali na wew unaona ni sawa kabisa hilo?

    ReplyDelete
  9. Unashindwa hata kuona kuwa wenzio wanalipwa ruzuku kila mwezi million mia mbili na kitu lakini wanashindwa hta kujenga makao makuu ya chama! wanashindwa hata kujenga kwenye kila jimbo waliloshinda ubunge ! matokeo yake wanafukuzana uanachama kwasababu ya kukataa kukaguliwa na mkaguzi mkuu halafu tena hawa watu kwa ujasiri kabisa wanataka nchi tena kwa kujinadi kuwa wana integrity? hyo imetoka wapi? watu kama wana uwezo wa kuchangisha mabilioni wakuyutumbua nchi Zima wakijinadi kuwa wako kwenye M4C kwanini wazichange hzo tukajenga mashule na mahospitali ingesaidia na hta wananchi wangewajaji kama ni watu wenye concern jamani nasema tena vichwa vyetu vinatumiwa vibaya sana !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Haya sasa ITV wameyakoroga na sasa watayanywa!

    ReplyDelete
  11. Nenda ccm huko kibaraka wao wewe tutakutukanasana nasiasa zako za wapuuzi.mlizoea kuburuza watanzania 2015 hiyo tutakutana kwenye Kura nukta.

    ReplyDelete
  12. Nachosikitika Ni kuwa Rangi tumeanza kutoa maoni hapa hakuna aliyeweza kunijibu kwa hoja zaidi ya kukurupuka benders fuuta upepo wenzenu tumesha kaa Sana kwenye hyo nikumbo mwisho tukaamua kutumia zetu akili.

    ReplyDelete
  13. Lello munama wewe mkali,wewe umetumia kichwa chako vizuri na umeona mbali sana,muombe MUNGU akuongezee busara zaidi.Ikiwa tu amemaliza muda wake wa uongozi na akjiongezea muda mwingine kiubabe je ni kweli kuna demokrasia hapo? Nikwamba hapa watu hawataki kuumiza vichwa vyao wanategemea wanasiasa ndio wawaongoze kwenye fikra zao wakiamini rais au mbunge ndiye atakaye mbadilishia maisha yake badala ya yeye kutumia akili yake,waache watukane weee mpaka wachoke.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad