October 18 2014 Wizara ya Afya ndio ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhusu kuwepo kwa mtu aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola kutokea wilaya ya Sengerema ambapo alikua ni binti wa miaka 17 mkazi wa kijiji cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema.
Alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili ambapo alilazwa kwenye Kituo cha Afya Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba 2014 kabla ya kuhamishiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema October 17 na kufariki duniani siku hiyohiyo saa 3.30 usiku.
Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo ndani ya siku ya 21 zilizopita ambapo alizikwa kama mgonjwa wa Ebola na hakukuwa na ndugu wala yeyote asiehusika isipokua Watu maalum waliokua wamevalia mavazi ya kujikinga.
Baada ya hapo Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilichukuliwa ili ithibitike ni ugonjwa gani umemuua sababu serikali iliahidi kutoa majibu hayo.
‘Hili swala la Ebola ni taarifa iliyotolewa bila kupitia kwenye mamlaka husika yani ilikua ni uvumi na huyo mtu aliezungumza kwamba kuna Ebola labda alikua anaona kuna dalili flani zimetokea akawa na wasiwasi lakini nikuhakikishie hatuna Ebola kwenye wilaya ya Sengerema’
‘Yule binti wa miaka 17 alieumwa mpaka akafariki alikua ana ugonjwa wa ini ambapo Wataalamu wanatuambia upande wa Afya kwamba mgonjwa wa Ini anapofikia hatua flani anaweza kupata dalili flani ambazo mtu anaweza kufikiria ni Ebola, tulijitahidi kuhakikisha kwamba hizo sampuli zimepelekwa kwenye Maabara Dar es salaam na taarifa tulizozipata ni kwamba hakuna kabisa dalili za ugonjwa wa Ebola kwa yule mgonjwa ambae alifariki‘ Mkuu wa wilaya Sengerema
Jibu la Serikali lililosubiriwa Baada ya Vipimo vya Ebola Kuhusu yule Binti wa Miaka 17 Aliefariki Sengerema
0
November 15, 2014
Tags