JK apiga marufuku kampeni, Ukawa wanasa waraka mzito

Wakati Rais Jakaya Kikwete akipiga marufuku vyama vya siasa na asasi za kiraia kufanya mapema kampeni za kuhamasisha wananchi kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umenasa waraka wa mkakati wa kutumia Sh2.5 bilioni za umma kuipigia debe katiba hiyo.

Pamoja na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa Dodoma, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein jana hiyohiyo, aliwataka Wazanzibari kuipitisha Katiba Inayopendekezwa bila kufanya makosa.

Nyuma ya kauli hizo za marais, Ukawa umesema umeandaliwa mkakati kabambe wa kuvitumia vyombo vya habari kwa fedha za umma kutoka Ikulu kuwashawishi wananchi kupigia kura ya ‘ndiyo’ katiba hiyo.

Kauli ya Rais Kikwete

“Kwa sababu hiyo naomba Watanzania wenzangu tuzingatie mamlaka ya Sheria ya Kura ya Maoni ambayo imeelekeza vizuri lini kura ya maoni itafanyika na lini kampeni zitafanyika, lini wadau watatoa elimu naomba tuwe na subira. Tukizingatia sheria hii hakuna ugomvi.”

Aliongeza hadi Tume itakapotoa maelekezo ya utekelezaji, wakati wa kampeni na kutoa elimu kwa umma bado na kwamba sheria ipo na imezipanga siku maalumu za kufanya hivyo.

Alisema licha ya sheria kuruhusu kampeni kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kura za maoni kupigwa, kwa mamlaka yake akiwa kiongozi wa nchi, kura na kampeni vitafanyika ndani ya siku 30 tu.

“Kampeni zitaanza tarehe 30 Machi na kumalizika tarehe 29 Aprili ikiwa ni siku moja kabla ya kupiga kura ya maoni. Muda huo ndiyo utakuwa wa kufanya hivyo,” alisema Kikwete.

 Waraka wa wapinzani

Jana, viongozi wa Ukawa walieleza kunasa waraka wa mkakati unaofanywa na Ikulu kutaka kuidhinisha fedha za umma Sh2.5 bilioni kwa ajili malipo kwa vyombo vya habari vitakavyotumika kushawishi wananchi kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa.

Tuhuma hizo ziliibuliwa jana kwa nyakati tofauti na Katibu Mwenza wa Ukawa, Dk Willibrod Slaa katika mkutano uliohusisha viongozi wenzake wa Ukawa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee katika moja ya mikutano yake Kanda ya Ziwa.

Viongozi wengine waliokuwapo kwenye mkutano wa Ukawa ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dk Slaa alisema mpango huo unaratibiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu.

Alisema Rweyemamu amepeleka dokezo hilo kwa Katibu wa Rais akitaka kuidhinishiwa kiasi hicho cha fedha ili kampeni za kushawishi wananchi zianze kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kazi ya kuelimisha umma itafanywa na kamati mbili zitakazoundwa na tume hiyo.

Alisema kabla ya kupiga kura ya maoni, Tume itaunda kamati mbili, moja itakuwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa kundi litakalopiga kura ya ‘ndiyo’ na ya pili kwa ajili ya elimu kwa kundi la ‘hapana’.

“Gharama za kamati hizo mbili zitakazoundwa maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa makundi hayo zitatolewa na NEC,” alisema Jaji Lubuva.
“Katika matangazo hayo kuna orodha ya wasomi 20 baadhi kutoka vyuo vikuu watakaokuwa wakishiriki kwenye mahojiano ambao kazi yao ni kueleza umuhimu kwa wananchi kuipigia kura ya ‘ndiyo’ Katiba Inayopendekezwa,” lilisema dokezo hilo huku likiwataja kwa majina baadhi ya wasomi hao.

Katika dokezo hilo, yametajwa majina ya watangazaji tisa wa televisheni ambao wataandaa vipindi kwa ajili ya `kuipigia debe’ Katiba Inayopendekezwa.

Lilisema kutakuwa na vituo vya redio 22 zikiwamo za kanda na mikoa ambazo zitafikisha ujumbe huo ili kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa.

“Umuhimu wa mpango huu ni kuiepusha Serikali na aibu ambayo inaweza kutokea endapo wananchi wataamua kuikataa Katiba Inayopendekezwa katika kura ya maoni,” Slaa alisoma sehemu ya dokezo hilo ambalo gazeti hili limeliona.

Alisema dokezo hilo linapendekeza kuwashirikisha wasanii wa kizazi kipya, makundi maalumu katika jamii, ngoma na vikundi vya utamaduni asili na magazeti yakiwamo ya udaku.

“Kundi la wahariri linaandaliwa kwa ajili kusaidia kuitangaza Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya magazeti, bajeti itajulikana baada ya kukamilisha mazungumzo na wahariri hao,” alisema Slaa akirejea dokezo hilo.

Alisema huo ni ufisadi wa fedha za walipakodi kutumika kupitisha Katiba ambayo haina manufaa kwa wananchi, bali kwa wanachama wa CCM.

“Hizi si fedha za Rais Kikwete, ni fedha za walipakodi wa nchi hii. Ikulu kutumia fedha hizi kwa ajili ya kushawishi wananchi ni ufisadi,” alisema.

Akizungumzia hilo, Mbatia alisema wakati Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikikosa Sh8 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa dawa, Sh2.5 bilioni zinatumika kupitisha Katiba yenye manufaa kwa wanaCCM na si wananchi.




Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. watanzania amkeni serikali ina deni kubwa MsD..INADAIWA PESA NYINGI MPAKA WAMEKAATAA KUSUPPLY DAWA MAHOSPITALI MAKUBWA YA SERIKARI MANA SERIKALI YETU NI PUMBAVU HAIANGALII WANANCHI WA CHINI..KIKWETEE ULAANIWE NA FAMILY YAKO SIKU UKIFA UTAZIKWA VIBAYA SANA HUTAENZIWA KAMA NYERERE KAMWE

    ReplyDelete
  2. huo n mtazamo wako, kwa hiyo wanaofanya vzur huwa wanataka wazikwe vizur

    ReplyDelete
  3. mhh yetu macho apandacho mtu ndicho avunacho,kwani mungu ni mjomba wa mtu?watu hawana hofu ya mungu kabisaa.msishangae kuona mtu anakuwa kichaa siwote wanaonewa wengine mungu analipa ataabike mpk kifo.hata magonjwa ooo huyu alikuwa mzima jamani kalogwa walahajalogwa ni malipo mungu analipa anaona akupe gonjwa uhangaikenalo mpaka kifo.maana ukiwa mzima hunahuruma nawanadamu wenzio so mungu anakupa lakuhangaikanalo vizuri.tumlilie mungu tu ndio hakimu wakweli natumuombe mungu 2015 tuchague kiongozi mwenye hofu ya mungu.ukiwa nahofu ya mungu huwezi kuwa mshenzi tuuu

    ReplyDelete
  4. Si ndio akili za sisi watu weusi akili pumba, hatujui kupambambanua kipi bora na manufaa kwa citizen, mtu hujui hupi mkono wa kulia wala kushoto, Citizen tunaitaji, huduma bora, madawa, good hospital. good schools, barabara nzuri, Usafi wa mazingira tunayoishi, walimu walipwe vizuri ili wafundishe watoto vizuri, elimu ni msingi bora wa kufuta ujinga, ndio hata Taifa letu litaonekana, taifa lililoendelea, Jamani wale Wazambia msiwaone wajinga kumuweka mtu mweupe kuwa raisi wao wamechoka na ujinga wa hao tunawaona ndugu weusi wenzetu kumbe ndio mbwa mwitu, wanatuweka katika wakati mgumu sana hawa watu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad