Kaka Yangu Anataka Kumuoa Mchumba Wangu, Ameamua Kwelikweli

Ndugu zangu kuna mchumba wangu mpaka sasa tuna mahusiano yenye umri wa miezi 5. 

Kaka yangu wa damu amekomaa kumchukua na kibaya jana kaniwahi kwenda kumtolea mahari(kiukweli kimapato ameniacha gepu sana), ndugu wa binti wamempokea tena vizuri. 

Nikimuuliza mchumba wangu kuna nini tena? Anadai naye hailewi kinachoendelea na ananishauri niwaishe mahari ndani mwezi huu.

Nikimuliza unamtaka nani ? Anadai amechanganyikiwa katika hili swala ila anadai kuwa bado ananipenda.

Ndugu zangu nifanyeje katika hili?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad