Hawa wadada wa mjini kujifanya wanauza nguo na simu kumbe uongo tu mwingine akamatwa....
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’ mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.
Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.
Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.
“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.
“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
Kigogo wa Madawa ya Kulevya wa Kike, Akamatwa na Madawa ya Kulevya
6
November 05, 2014
Tags
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteMPAKA TABATA KIMANGA MATEJA KIBAO MPAKA HURUMA NA SEGEREA NENDENI WAMEKUWA WANABEBA WANAZUGIA WANAUZA NGUO NA MAPOCHI, KUMBE WANAHARIBU VIJANA,
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletena wewe administrator muogaaaa,tunawataja wauza sembe unaogopa watakumaliza?unafuta comment nyoooooo,kama Mungu kakuandikia utakufa kupitia mkono wa wauza sembe,aina ujanja kifo chako kinapangwa na Mungu pekee,acha uoga
ReplyDelete