Kikao kinaongozwa na Wasira na Lukuvi,
Wabunge wa ccm wale wanaopiga kelele kuhusu Wizi huu wamewekwa mtu kati,
Kinafanyikia Ikulu ya Dodoma kwa siri kubwa, hata magari yao yote yameigizwa ndani kabisa, kwa hapa nje lipo Gari la Lembeli aina ya Range Rover Namba T382 lililokosa nafasi ndani. kikao hiki kimeitishwa kwa meseji tu hii ni baada ya jioni kutangazwa kuwa kimeahirishwa,
Sababu za usiri huu ni pale tulipowaanika jana katika kikao chao cha shinikizo kwa Werema ajiuzuru, Zigo limemdondokea Godfrey Zambi kuwa ndie aliyevujisha siri ile kwakuwa aligoma kuzima simu na alikuwa akichati fb wakati kikao kikiendelea, hivyo kikao cha sasa hivi katupwanje.
Kikao hiki kwa sasa kimembana Ndugai kwamadai anaihujumu serikali,
Ndugai amezila kuendelea na Bunge amesema yeye sasa hata ongoza vikao, bora awe pembeni kuepusha msongamano!
Ccm imegawanyika makundi matatu, lile linaloshinikiza waliohusika na wizi huu wote wapigwe chini lakini,ukifuatilia kundi hili linavizia vyeo vya uwazili, na tayari kampenzi za kuwania vyeo hivyo zimeanza.
Kundi la pili hili ni wanafiki wa kati wasio na msimamo, lenyewe linataka wafukuzwe wachache (maswi,tibaijuka,mhongo na werema) hili linasema linanusuru serikali isianguke.
Kundi la mwisho ni la wezi wenyewe, hili linafanya kila njia ripoti hii isisomwe bungeni, hili linaongozwa na Pinda na Werema.
UPDATES.22/11/2014
Ndege ya serikali ipo hapa Dodoma imekuja alfajiri hii 5-H CCM.. Aina ya folker F28 haijajulikana imemleta au imekuja kumchukua Nani, ila taarifa za awali zinasema Bilali alikuwa aje leo.
Hali ya mambo ni ngumu kama vile nchi ipo vitani...!
Kinana tayari ameletwa na Ndege mida hii,
Mrejesho wa Kikao Cha jana usiku
Imeamriwa popote alipo Spika Makinda aje, Ndugai out hadi sakata lipite, afanye awezavyo Pinda apone,.. Wachangiaji wakali wasipate nafasi iitwe briefing ya wabunge wote watapike nyongo nje ya waandishi ili siku ya mjadala kuwe na hewa safi.Kama ni kuondoka waondoke mawaziri ila sio waziri mkuu.
Inatakiwa njia ya kumuangukia au kumdhibiti Mh. Mengi wa IPP,
Leo agenda kuhusu Mengi itajadiliwa kwa kina katika kikao cha baadae. Ifahamike kuwa Vyombo vya habari vya Bwana Mengi vimekuwa vinalielezea jambo hili kwa uwazi na uhuru mkubwa kiasi cha umma kulielewa.