Kucha za Bandia zile za Kubandika na Gundi Samsababishia Mauti Bibi Harusi


“Sijui walitumia gundi ya aina gani
kumbandikia kucha mwanangu, mpaka sasa sielewi, mtoto mwenyewe ndiyo huyo huyo mmoja wa kike niliyekuwa nikimtegemea na ndiyo kwanza ndoa yake bado change kabisa hata mwezi mmoja haina, huu ni mtihani mkubwa kwangu na kwa mumewe ambaye wamefunga naye ndoa wiki tatu zilizopita, inauma sana lakini
tunamwachia Mungu.”

Ni maneno ya mama mzazi wa Sophia Komba aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es Salaam, baada ya kupata kidonda kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto alipokuwa akibandua kucha za bandia alizobandikwa siku ya harusi yake na kusababisha apatwe na tetenasi.
Sophia hadi kifo kinamkuta alikuwa na umri wa miaka 28, Oktoba 15 alifunga ndoa na Richard Mmary katika harusi ya aina yake iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wakisimulia namna walivyomuuguza Sophia kwa takriban wiki moja na
nusu, mume wa marehemu anasema
wiki moja baada ya sherehe ya harusi yao, Sophia aliamua kwenda tena salon kwa ajili ya kutengeneza nywele na kutoa kucha alizobandikwa siku ya harusi yao.
“Ilikuwa siku ya Jumamosi jioni,
Sophia aliniaga anaenda saluni, alirudi baada ya saa mbili kupita lakini alikuwa akilalamika kuwa kidole kinamuuma sana, nikamuuliza amefanya nini akanijibu kuwa alikuwa anabandua kucha, lakini bahati mbaya kucha moja inaonekana ilibandikwa vibaya walipokuwa wanaibandua ilibanduka na ngozi ya pembeni ya kidole na ikamuachia kidonda.
“Sikujali sana nikajua ni kidonda cha
kawaida tu, nikaenda kwenye duka la dawa nikamnunulia spiriti
nikamsafisha lile eneo, lakini
kilichonishangaza alikuwa akilalamikia maumivu makali,” anasema.
Mama yake Sophia, Victoria Haule
anasema kuwa anaamini kuwa kifo cha mwanaye kimetokana na kucha bandia ambayo ilimsababishia apatwe na
tetenasi.
“Tulipoona maumivu yanamzidia,
tulimpeleka Hospitali ya Sinza, daktari alipomfanyia vipimo alitutaka tumpeleke Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi, kwa kuwa alibaini kuwa Sophia ana tetenasi iliyosababishwa na kile kidonda.
Binafsi niliamini kucha ile ndiyo
tatizo, kwa kuwa ilifikia hatua mkono
mzima ukawa umevimba na
kubadirika rangi na kuwa mweusi sana kama damu imevilia,” anasimulia mama yake Sophia.
Kwa maelezo ya ndugu hao wa
marehemu, Sophia alifariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu na kwa
mujibu wa daktari kifo chake
kilisababishwa na tetenasi.
Mabibi harusi wengi hivi sasa na hata wanawake kwa wasichana
wanapendelea sana kubandika kucha bandia wakilenga kuboresha
mwonekano wa vidole vyao. Wengi
hupenda kuwa na kucha ndefu ambazo huzipaka rangi na hivyo kuvutia pindi mtu azionapo.

Top Post Ad

Below Post Ad