Iliripotiwa kuwa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni ililikabidhi suala la utata wa Miss Tanzania 2014 kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kufanyiwa uchunguzi.
Pia ilidaiwa kuwa BASATA lina siku 7 za kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa utata uliojitokeza. Habari hizi za uchunguzi zilijulikana takribani wiki mbili zilizopita.
Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zozote zile juu ya kilichojulikana kutokana na uchunguzi huo. Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni alinukuliwa akisema kwamba "Tayari tumeshalikabidhi kwa BASATA na tumewapa muda wa wiki moja kisha watatupa majibu na ushauri juu ya walichogundua, baada ya hapo sisi tutajua nini kifanyike na kutoa tamko rasmi"
Sasa huu ukosefu wa tamko rasmi tuutafsiri vipi? Ndo yale yale ya 'huu ni upepo tu, utapita' au...? Manake hii habari ndo imeshajifia zake na ni kama vile hakuna tena mwenye raghba ya kutaka kujua au hata kufuatilia ili kuweza kujua hatma yake!
Je, ndo Watanzania ndivyo tulivyo - wepesi sana wa kusahau mambo na hatuna hulka ya kufuatilia mambo mpaka tukajua mwisho wake? Au tunasumbuliwa na maradhi ya ukosefu wa nadhari?
Kuhusu Miss Tanzania 2014, Ndiyo Tumeshasahau au inakuwaje Hasa?
1
November 08, 2014
Tags
Yan wanaleta mambo kibao ili lisahaulike,ila asubirie mic world huyo bibi bomba asione watu wametulia akahisi wamemfurahia
ReplyDelete