Lemutuz:Waliopokea Pesa za Escrow ni Wezi kama Wezi Wengine wa Kuku na Mbuzi Warudishe Haraka Sana

Well, mwisho wa yote kuna Viongozi wengi wametajwa kuhusika na kupewa pesa za Escrow na hakuna aliyetajwa kuzikataa na so far sijaona popote inaposemwa kwamba kazi waliyoifanya ili kupewa na kupokea pesa hizo, na naomba niwe mkweli kati ya wote walioatajwa kupokea pesa hizo nimeshitushwa sana na Wawili, yaani Waziri Mama Tibaijuka na Askofu Kilaini I mean wengine sikushitushwa sana maana some of them tumewazoea na habari za rushwa all the times.

Mama Tibaijuka, hivi kweli anaweza kusimama mbele ya umma na kusema pesa alizopewa sio chafu? Hivi ni kweli alipokuwa UN aliwahi kupokea pesa za namna hiyo? Sasa kwa nini anakuja kupokea akiwa Waziri wa CCM? Askofu Kilaini hata na yeye naye anaweza kweli kukubali kupokea Shillingi Millioni 80 bila ya kuzifanyia kazi inawezekana vipi? Hizi pesa walipewa za Rushwa nia na madhumuni ilikuwa kuwanunua their influence, wamekamatwa red handed tunapoteza muda kujadili bungeni kujadili nini na ukweli upo wazi kuwa wamepewa pesa na wamezipokea!

- Kwanza warudishe hizo pesa kwa waliowapa, and then hatua za kinidhamu zichukuliwe na hasa kutoka kwa Chama cha Mapinduzi, wale wote walio wanachama wa CCM waliopokea hizo pesa chafu wachukuliwe hatua na ikibidi waende Mahakamani kwa kupokea Rushwa, huyo Askofu watajijua wenyewe huko Kanisani kwake ila I hope hatahubiri tena ila ndio maana sijawahi hata kumsikiliza nilishamshitukia siku nyingi kuwa hayupo kwenye mstari na Mungu, wanajifanya kupiga piga kelele za siasa kumbe wanatafuta mlo tu na hizi siasa za kuwachanganya Maaskofu sijui tumezianza lini Tanzania.

- Warudishe Pesa chafu ni za Rushwa na halafu waadhibiwe na CCM and then Sheria ichukue mkondo wake si kuna Rushwa hapo!!

Le Mutuz
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad