Maruhani Yamsumbua Penny, Apiga Makelele Barabarani Ovyo

Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani.

Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenzi aitwaye Skitter alifariki dunia.

Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo. Mpashaji wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama  dakika kumi, Penny aliondoa gari na kuendelea na safari.

Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa rafiki yake, alipokaribia kufika alipata uchungu ndiyo akatokewa na hali hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad