Mchumba wa Agness Masogange Aibuka na Kusema Haya Kuhusu Kusalitiwa

STORI: Musa Mateja
MCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ aitwaye Evance Kom juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa msichana huyo amemsaliti baada ya kuvunja makubaliano yao.
Akizungumza na gazeti hili Jumatatu hii, alisema hana tena mpango wa kuoana na Agnes kwani kitendo chake cha kuamua kuhamia Afrika Kusini kimeonyesha wazi hawawezi kuishi tena pamoja.Akisimulia, Evance alisema hapo awali walikubaliana kuwa pamoja kiasi kwamba hadi kufikia kumvalisha pete, wazazi wa pande zote mbili walikwishajua na kubariki uhusiano wao.

“Wakati anapanga mipango yake ya kuhamia Afrika Kusini, hakuwahi kuniambia hata mara moja, alikuja kuniambia eti tuhamie huko siku chache tu kabla hajaondoka, nisingeweza kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya huko wakati hapa Bongo nina miradi yangu kibao,” alisema.

Alisema kutokana na kitendo hicho cha kuhamia huko, pia mchumba wake huyo alikuwa amejiingiza kwenye mambo yasiyofaa ambayo wazazi wake wasingeweza tena kumsapoti kama angehitaji kuendelea na nia yake ya kumuoa.

“Nilimpenda sana Agnes na yeye alinipenda lakini alichokiamua ni kizuri kwake, ila kwangu ni kama amenisaliti maana kajiingiza kwenye mambo yasiyofaa hivyo kwa sasa amebaki kama rafiki yangu wa kawaida tu,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad