Leo katika taarifa ya habari saa 1 jioni ya kituo cha televisheni cha K24 cha Kenya imeonesha mchakato wa usajili na uandikaji namba mpya za magari nchini humo, uandishi wa vibao vya namba za magari unaofanywa na wafungwa wa gereza nchini humo.
Uandishi wa vibao vya namba za magari ni mradi endelevu tena wenye kuingiza fedha nyingi mno. Kwa hapa kwetu,mradi mara ya kwanza ilipewa kampuni binafsi. Inasemekana kampuni hiyo ina ubia na Waziri Mkuu wa zamani,ambaye ni fisadi mjanja sana. Ameificha miradi yake ya kifisadi kwenye majina na makampuni yaliyochini ya watu tofauti tofauti.
Hapa nchini,makampuni yenye kuzaa faida yamechukuliwa na viongozi mafisadi,mfano,makampuni ya mawasiliano yalichotwa hisa za umma kupewa wageni kwa niaba ya mafisadi wazawa walio ndani ya Serekali, angalia TTCL,ATCL, aidha, inasemekana tiGO ilipokuwa chini ya MIC ltd serikali ilikuwa na hisa % 17 ambazo zilichotwa kinamna na spika mmoja wa zamani wa bunge la JMT.
Huko Kenya kampuni ya simu ya umma ndiyo inashikilia na kutamba katika nyanja ya mawasiliano nchini humo.
Kwa mfumo huu, Kenya itendelea kututimulia vumbi.
Moja ya Sababu ya Kenya kuwa Juu ya Tanzania Kiuchumi
0
November 19, 2014
Tags