Mtekaji na Muuaji wa Watoto Ifakara Akamatwa na Polisi, Wananchi Wachoma Nyumba Yake

Polisi hapa mjini Ifakara wamepata wakati mgumu kumwokoa bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Nurdin Mangula, baada RAIA wenye hasira Kali kutaka kumuua wakimtuhumu kuiba watoto na kuwaua kisha kuchukua baadhi ya viungo na kuviuza kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Jamaa huyo ambaye mke wake ni hakimu wa mahakama ya mwanzo aliokolewa na polisi waliotumia nguvu kubwa kumnusuru asiuawe na RAIA wenye hasira Kali.

Tukio hilo lililotokea jana saa 10 jioni, lilivuta watu wengi na kuifanya polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya watu hao. 

Wiki mbili zilizopita kuna watoto wawili walipotea katika mazingira ya kutatanisha na mmoja kupatikana akiwa tayari ameshakufa na baadhi ya viungo akielwa hana. 

Mtuhumiwa huyo ambaye ana undugu na makamu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula amekutwa na watoto watatu kwenye gari aina ya Noah na mmoja akiwa tayari amekufa.

Pamoj na kuokolewa na polisi watu wamefanikiwa kuichoma moto nyumba yake na magari mawili. kuchukua kila kitu ndani ya nyumba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad